Mbunge wa jimbo la kalenga Jackson Kiswaga akikagua timu wakati wa nusu fainali ya ligi ya mkoa wa Iringa (Asas super league)
*************************************************
Mbunge wa jimbo la kalenga Jackson Kiswaga anatarajia kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwenye jimbo hilo kuanzia mwezi wa tano mwaka huu kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo wa jimbo hilo.
Akizungumza kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali wa ligi ya mkoa wa iringa (Asas super league) baina ya Kidamali na Ivambinungu fc,Kiswaga alisema kutokana na hamasa ambayo wanamichezo wanayomichezo wa jimbo hilo anapaswa kuanzisha mashindano hayo kwa lengo la kukuza vipaji hivyo.
Kiswaga alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa yakifanyika miaka ya nyuma na yalikuwa yanazalisha vipaji vingi na yaliongeza ajira kwa wadau mbalimbali.
Kiswaga alisema kuwa michezo kwa sasa ni ajira rasmi ambayo imekuwa kiwanda ambacho kinazalisha ajira nyingi kwa sasa kulingana na soko la ajira.
Alimalizia kwa kuzipongeza timu zote zinazoshiriki ligi ya mkoa wa Iringa ( Asas super league) hadi kufika hatua ya nusu fainali.