NA DENIS MLOWE,IRINGA
TIMU ya soka ya Mtwivila (Ifuenga United) imeshindwa kutamba katika mchezo wa nusu fainali ya pili baada ya kulazimishwa sare ya 0 – 0 dhidi ya Irole Fc katika uwanja wake wa nyumbani wa Kalenga.
Mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali toka dakika ya kwanza ya mchezo na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki kutoka Kijiji cha Kalenga.
Wakishangiliwa na mashabiki wao Ifuenga United licha ya kutawala mchezo huo walishindwa kutumia vyema nafasi walizopata kwa washambuliaje wake Kukosa umakini kila wakifika golini kwa wapinzani wao.
Hadi mwamuzi wa mchezo huo Makuka akipuliza kipenga Cha kipindi Cha kwanza Hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Kipindi Cha pili licha ya timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji Hali iliendelea hivyo za kila timu kushindwa kutumia vyema nafasi walizopata katika mchezo huo.
Hivyo Mara ya mchezo kumalizika timu itakayoingia fainali inatarajiwa katika mchezo wa nusu fainali ya pili kwenye mchezo utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Mkwawa.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Mkwawa badala ya Irole kutokana na timu ya Irole fc kufungiwa kucheza kwenye uwanja wao kwa sababu ya matukio mbalimbali ya mashabiki wao kutokuwa rafiki kwa timu pinzani.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya maziwa ya Asas ya mjini Iringa bingwa ataondoka na kitita Cha sh milioni 2 ,jezi, mipira na Cheti Cha kushiriki mabingwa wa mkoa, mshindi wa pili ataondoka na sh milioni 1 jezi na mpira wakati mshindi wa tatu atajinyakulia laki 5
Aidha kutakuwa na Zawadi kwa mchezaji Bora wa mashindano,mwamuzi Bora,mfungaji Bora na timu yenye nidhamu.