Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashugwa akizungumza na wamiliki wa vyombo vya habari na Wamiliki wa Kampuni za Visimbuzi Leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Innocent Bashugwa akipata maelezo ya simu zilivyotumika zamani kutoka kwa Mhifadhi Mwandamizi wa Makumbusho wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Raphael Mwango wakati waziri huyo alipoafanya ziara katika Makumbusho hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashugwa akizungumza katika Makumbusho ya TCRA na kudai Mamlaka imepangilia Makumbusho hayo.
Picha ya mbalimbali za Makumbusho TCRA.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano wa wadau wa Wamiliki wa vyombo vya Habari na Kampuni za Visimbuzi Jijini Dar es Salaam.
Wadau wakichangia mkutano kuhusiana na sekta ya utangazajiKaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Joannes Karungura akitoa akizungumza kuhusiana na masuala ya utangazaji katika mkutano wa wadau wa vyombo vya habari vya utangazaji na wamiliki wa kampuni za visimbuzi.
**********************************************
WAZIRI wa Habari,Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema kuwa mfumo wa dijital una nafasi kubwa ya mapato hivyo vyombo vya habari vinaweza kutumia fursa katika kuatangaza bidhaa mbalimbali katika kanda.
Hayo aliyasema Waziri wakati alipokutana na Wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na wamiliki kampuni za visimbuzi pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni ziara ya kukutana na wadau kujadili masuala mbalimbali ikiwemo na changamoto mkutano wa wadau hao umefanyika Makao Makuu ya TCRA
Amesema kuwa kukutana na wadau ni hatua iendelevu aliyopanga katika kuangalia vitu mbalimbali vya sera pamoja na sharia kwa lengo ya kukuza sekta ya habari na utangazaji nchini.
Bashungwa amesema kuwa maoni ya wadau watayafanyia kazi na kuwataka kuendelea na majadiliano ya mara kwa mara na wadau wa utangazaji kuingia katika mfumo mmoja wa kuwa na king’amuzi kimoja kwa siku zijazo.
Aidha Bashungwa amesema kuwa mapato mengi yanapotea kutokana mifumo ikiwemo kwa wasanii kupata haki zao.
Waziri Bashungwa katika ziara hiyo pia alifanya ziara katika Makumbusho ya TCRA na ambapo alisema ni sehemu nzuri ya watu kujifunza historia ya Mawasiliano tangu ilivyoanza.
Amesema kuwa katika Makumbusho hayo watengeneze na kuweza kutangaza ambapo Mamlaka hiyo ilishaanza kufanya hivyo.
Waziri huyo amezungumza na Cosota,Basata na TCRA kuangalia wanavyoweza kufikia malengo ya Serikali katika kutangaza Tanzania Pamoja na kujadili maslahi ya wasanii.