
Waamuzi na manahodha wa mechi ya kwanza ya nusu fainali Kati ya Ivambinungu na Kidamali
**********************************************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
TIMU ya Soka ya Ivambinungu Fc ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa iko mguu ndani mguu nje kuingia fainali ya ligi soka daraja la tatu inayojulikana kwa jina la Asas Super League baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1 – 0 dhidi ya Kidamali katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa ligi hiyo.
Mchezo huo wa kwanza uliopigwa katika uwanja wa Wambi Mjini Mafinga ulikuwa mkali na wa kusisimua vipindi vyote viwili kwa kila timu kutaka matokeo makubwa kujihakikishia kuingia fainali.
Licha ya timu zote kuonyesha kiwango kikubwa Cha mchezo kwa vipindi vyote Hadi kipindi Cha kwanza kinaisha Hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Kipindi Cha pili kilianza kwa Kasi kubwa huku timu ya Ivambinungu Fc wakionyesha mpira wa darasani na huku wakishangiliwa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo.
Ule wakati uliosubiliwa na mashabiki ulifika ambapo katika dk ya 87 ya mchezo mshambuliaji hatari Wille Chang’a wa Ivambinungu aliwainua vitini na kuandika bao la kwanza na la mwisho katika mchezo huo.
Mchezo wa nusu fainali nyingine itazikutanisha timu ya soka ya Irole fc siku ya kesho na Ifuenga United (Mtwivila Fc) katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kalenga.
Bingwa wa ligi hiyo inayoyodhaminiwa na kampuni ya maziwa Bora nchini ya Asas ataondoka na milioni 2 kikombe cha ubingwa, seti za jezi na mpira na uwakilishi wa kushiriki mabingwa wa mkoa, mshindi wa pili milioni 1, mshindi wa tatu laki tano.