Mgeni Rasmi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga (kushoto), akisalimiana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Zimamoto Saccos Ltd Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha BOT Jijini Mwanza Mapema leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zimamoto Saccos (SACF) Christina Sunga (kushoto), akitoa neno na kumkaribisha Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Zimamoto Saccos Ltd uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha BOT Jijini Mwanza mapema leo asubuhi.
Mgeni Rasmi Kamishna Jenerali (CGF) John Masunga, (kushoto) akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Zimamoto Saccoss LTD uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha BOT Jijini Mwanza mapema leo asubuhi.
Baadhi ya Wajumbe walishiriki kikao cha Mkutano Mkuu wa Pili wa Zimamoto Saccoss Ltd
Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga (aliyekaa katikati) na baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha Mkutano Mkuu wa Zimamoto Saccos Ltd uliofanyika katika Chuo cha BOT Jijini Mwanza mapema leo asubuhi.
Mgeni Rasmi na Mlezi wa Zimamoto Saccos Ltd, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga (kulia) akipokea cheti cha umiliki Hisa kwenye Zimamoto Saccoss katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Zimamoto Saccos Ltd uliofanyika katika Chuo cha BOT Jijini Mwanza mapema leo asubuhi. (Picha zote na Mjumbe wa Zimamoto Saccos Ltd)
……………………………………………………………………………………….
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mlezi wa Zimamoto Saccos (CGF) John Masunga amezindua Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka wa Zimamoto SACCOS LTD 2021 unafanyika Mkoani Mwanza, katika Mkutano huo ulioshirikisha wanachama na wajumbe zaidi ya 124 waliotoka mikoa mbalimbali wakiwawakilisha maafisa na askari wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali Masunga alizindukia kikao hicho mapema leo asubuhi na aliwataka Makamanda wa Mikoa ambao ndiyo Walezi wa Zimamoto Saccos mikoani, kuhakikisha wanawashawishi Maafisa na askari ambao hawajajiunga wajiunge, ili kutatua changamoto walizonazo.
“Maafisa na Askari wengi wanakosa pakukimbilia wanapokuwa na matatizo haswa ya kifedha, wanaenda kukopa kwenye taasisi nyingine za kifedha kwa riba kubwa, muwashawishi kwa kuwaelimisha watumishi wetu ili wajiunge na Zimamoto Saccos” Alisema Kamishna Masunga.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Zimamoto Saccos (SACF) Christina Sunga amewataka wajumbe ambao bado hawajatimiza vigezo vya kuwa Mwanachama halali wa Zimamoto Saccos wahakikishe wanatimiza vigezo.
Christina Sunga alisema mpaka sasa tuna Wanachama Zaidi ya 207 lakini kati ya hao ni wanachama nusu tu ambao wametimiza uhalali wa kuwa wanachama wa Zimamoto Saccos. “Tujitahidi kuhimizana sisi wenyewe ili idadi hii itimie na tuweze kuongeza wanachama wengine” alisema Mwenyekiti wa Bodi Christina Sunga.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho wameahidi kuwa mabalozi kwa Maafisa na Askari ili wajiunge na Zimamoto Saccos Ltd, pia wale ambao bado hawajatimiza kuwa wanachama halali wa Saccos, wameahidi watahakikisha baada ya kikao hiki watatimiza matakwa ya Zimamoto Saccos kwa kumalizia hisa wanazo daiwa.