Naibu Katibu Mkuu, Bw. Gerald Mweli, akikagua moja ya Vyoo katika Shule ya Msingi Kagera na kutoa maelekezo na kutoa maelekezo yakuvitunza Vyoo hivyo
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (E), Gerald Mweli, akikagua moja ya Vyoo katika Shule ya Msingi Kagera na kutoa maelekezo yakuvitunza Vyoo hivyo.
…………………………………………………………………….
Na Atley Kuni, Ukerewe, MWANZA
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba, wanaotarajiwa kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza tarehe 11 Januari, 2021 wanajiunga elimu hiyo ya Sekondari bila kukosa.
Mkuu wa Wilaya ya ukerewe Mhe. Cornel Magembe, akimuelezea hali ya elimu wilayani humo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI anaye shughulikia elimu Gerald Mweli, alisema watoto wote waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2021 wataingia Sekondari bila kukosa.
“Naibu Katibu Mkuu, naomba nikuhakikishie kuwa, watoto wote 8184, waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka huu, sisi kama Wilaya hatuna wasiwasi, kwakuwa wote wataingia kuanza masomo yao bila kukosa, kwani tumejipanga na tuna vyumba vyakutosha kwa ajili ya wkuwapokea bila kuacha hata mmoja, na ndio maana utaona sisi katika Wilaya yetu, hatuna mamabo ya chagua la pili.”alisema Magembe.
Mbali yakuelezea juu ya maandalizi yakuwapokea kidato cha kwanza, Mkuu huyo wa Wilaya, hakusita kufikisha ujumbe wake kwa kiongozi huyo kuhusiana na kujidhatiti kwakujenga jumla ya vyumba zaidi ya 300 kwa nguvu za wananchi na hivyo wanahitaji nguvu ya ziada ya Serikali kuu kwaajili yakukamilisha ili vianze vyumba husika vianze kutumika.
Akijibu maombi hayo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Geraid Mweli, ambaye yeye na ujumbe wake wapo wilayani humo kwa ziara za kikazi, alimhakikishia Mkuu huu huyo wa Wilaya kuwapa ushirikiano wakutosha ili malengo waliojiwekea yaweze kutimia.
“Mhe. Mkuu wa Wilaya kwanza niwapongeze kwa hatua kubwa mliyopiga katika Nyanja ya elimu, ninyi ni mfano wa kuigwa, siwezi kusema vyumba vyote 200 mlivyo omba kuwasadia itakuwa hivyo, lakini kwa kadri itavyo wezekana tutajitahidi kupitia Programu mbali mbali kama EPforR na Seqiup, lakini tunaposema Serikali ni pamoja na ngazi ya Halmashauri, hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri lazima naye alione hili”. Amesema Mweli.
Naibu Katibu Mkuu Gerald Mweli, yaupo katika ziara ya kikazi wilayani humo, ambapo pamoja na mambo mengine, ametumia fursa hiyo, kukagua, kuzindua miradi ya madarasa ya elimu maalum na kuongea na watumishi walimu na waratibu elimu kwenye Wilaya hiyo.