MKURUGENZI wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (MB) akiwasilisha mada ya lishe kwenye semina ya Madiwani wa Halmashauri ya Muleba iliyoandaliwa na Shirika hilo |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Emmanuel Sherembi akizungumza jambo wakati wa semina hiyo |
MGANGA
Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Modest aliwasilisha mada ya Lishe kwa
Madiwani hao ambapo semina hiyo iliandaliwa na Shirikala Agri Thamani
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Muleba Emmanuel Sherembi akizungumza jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Neema Lugangira (MB) |
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Muleba Emmanuel Sherembi
KATIBU wa CCM wilaya ya Muleba akisisitiza jambo kwa Madiwani kuwa lazima ajenda ya lishe itekelezwe na waipe kipaumbele maana ipo kwenye ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2021 |
Baadhi ya Madiwani wa wilaya ya Muleba wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina
MRATIBU
wa Lishe kutoka Tamisemi Mwita Waibe na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba
Dkt Modest Mganga wakifurahia namna ambavyo semina ya Lishe imeendeshwa
MKURUGENZI
wa Shirika la Agri Thamani Mh Neema Lugangira (MB) akigawa nakala ya
mada kwa madiwani iliyokuwa inawasilishwa na Idara ya Afya ya
Halmashauri ya Muleba
SHIRIKA la Agri Thamani Foundation
limewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kuendelea
kubeba ajenda ya lishe kwenye maeneo yao ili kuweza kudhibiti hali ya udumavu
katika wilaya hiyo.
Semina hiyo imewafikia Madiwani wa Kata ,Madiwani wa Viti Maalumu kutoka Kata zote 43 za wilaya ya Muleba.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Agri
Thamani Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Tanzania Bara anayewakilisha
Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.) wakati
akizungumza na Madiwani, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Wakuu wa Idara wa
Wilaya ya Muleba wakati wa Semina ya Lishe iliyoandaliwa na Agri Thamani.
Amesema kuwa ili kupunguza udumavu
katika wilaya ya Muleba ni kuhakikisha wananchi wanajikita katika mazao lishe
pamoja na viongozi hao kushirikiana na watalaam wa lishe na kilimo ili kwenye
vikao vya ngazi zao kuweza kutoa elimu iliyosahihi.
Mbunge Neema Lugangira ameongeza
kuwa viongozi hao wanatakiwa kushirikiana na watalam wa afya kutoa tathimini ya
mara kwa mara kuhusu hali ya lishe kwenye maeneo yao kwani watalam hao hawawezi
kuingia sehemu zote kwa wakati mmoja.
“Sisi sote tuna jukumu la kujua
hali ya lishe, udumavu n.k. tunapaswa kuangalia katika mtaa wetu, katika kijiji
chetu hali ikoje ya lishe na tukikumbana na hali ya lishe duni na viashiria
vyake tunatoa taarifa kwa wenzetu upande wa serikali” Alisema Mhe Neema
Lugangira (Mb.)
Naye
kwa upande wake,Mratibu wa
Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mwita Waibe aliwaambia Madiwani kuwa
Tamisemi imekuwa ikishirikiana na Agri Thamani kwa karibu huku
akilipongeza Shirika hilo kutokana na kwamba ni NGO ambayo inafanya kazi
za jamii na kuzifikisha ngazi ya
jamii.
Mratibu Mwita aliwasisitizia madiwani wa Halmashauri hiyo waendelee kuyatafsiri mafunzo haya kwa vitendo ili Agri Thamani
iweze kupata msingi wa kuandaa Programu zitazoshuka hadi ngazi ya vijiji.
Kwa upande mwingine, Katibu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muleba Agnes Kassela aliwataka Madiwani wa
Halimashauri ya Wilaya ya Muleba kwa kutekeleza maagizo hayo kuhusiana na Ajenda nzima
ya Lishe kama ilivyo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 kwani
sasa ni muda wa utekelezaji na wao ndio wasimamizi wakuu wa miradi ya
maendeleo.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Halamshauri ya Muleba Bwana Justus Magongo ameiliishukuru Shirika la Agri
Thamani kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Madiwani kwa kuwapatia elimu hiyo ya
lishe ambayo ni muhimu sana.
Alisema watahakikisha wanabeba
ajenda ya lishe kwa vitendo kwenye Halmashauri hiyo kupitia vikao vyao na
mipango kazi ili kuweza kupunguza kiwango cha udumavu katika Wilaya hiyo.