Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akizindua kampeni maalum ya upandaji Mti ambapo amesema kila mtumishi wa umma kupanda miti kumi kila wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga,akipanda mti eneo la Medeli zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru akipanda mti katika eneo Medeli zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge
Afisa Lishe Mkoa wa Dodoma, Heriet Carin,akipanda mti katika eneo la Medeli zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge
Wanafunzi kutoka UDOM wakipanda mti katika eneo la Medeli zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge
Watumishi mbalimbali na Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma wakipanda mti katika eneo la Medeli zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge,akizungumza na watumishi na wageni walikwa waliohudhuria zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Januari 9,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge,akisisitiza jambo mara baada ya kuongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Januari 9,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga,akizungumza jinsi walivyojipanga kuitunza miti hii ili iweze kustawi na kulipendezesha jiji la Dodoma mara baada ya kupanda miti katika eneo la Medeli leo Januari 9,2021.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Bilinith Mahenge kwa kuongoza zoezi la upandaji miti katika eneo Medeli jijini Dodoma leo Januari 9,2021.
Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro,akielezea jinsi walivyojiwekea sheria ndogo za utunzaji na usimamizi wa Mazingira za Jiji la Dodoma zimesambazwa katika Kata na Mitaa ili kudhibiti mifugo leo Januari 9,2021.
Mtunza Hazina wa Chama cha Mazingira kutoka UDOM ambaye pia ni Mwenyekiti wa TAKUKURU Washington Sabuyi,akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa mwaliko walipewa wa kupanda mti zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Januari 9,2021.
……………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,ameagiza kila mtumishi wa umma kupanda miti kumi kila wiki huku akizitaka halmashauri zote kutenga maeneo ya upandaji Miti.
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dodoma wakati akizindua kampeni maalum ya upandaji Miti amesema kuwa kila mtumishi apande miti kumi kila wiki ili kurejesha uoto wa asili pamoja na kuliweka jiji katika mazingira bora.
”Hivyo nawataka wakurugenzi wa halmashauri zote nane za mkoa wa Dodoma kutoa orodha ya watumishi ambapo kila mmoja atahusika kupanda miti na kumi kila wiki kwa utaratibu atakaojiwekea huku akiagiza kupatiwa ripoti ya kampeni hiyo kila ifikapo siku ya Jumatatu”amesema Dkt.Mahenge
Aidha Dkt.Mahenge ametaka miti hiyo kuwekewa alama au jina mtu aliyepnda ili iwe rahisi kutambulika pamoja na utunzaji wa mti huo hata mimi nimepanda miti 22 hivyo nataka iwekewe alama ili niweze kuitunza vizuri
”Katika kulifanya zoezi hilo kuwa na umuhimu nashauri watumishi wanaweza kushirikisha familia au marafiki zao katika kupanda miti hiyo. Utekelezaji wa zoezi hilo utakaguliwa na kuingizwa katika taratibu za kiutumishi ili iwe rahisi kuchukua hatua”amesisitiza Dkt.Mahenge
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga,amesema kuwa upandaji huu wa miti katika jiji la Dodoma ni mwendelezo wa maagizo ya viongozi wakuu wa kitaifa na maagizo yako ya Mkoa tunatekeleza maagizo hayo.
”Sisi katika wilaya yetu ya Dodoma tunatekeleza zoezi hili jambo kubwa ni utunzaji wa miti hii kama ulivyosikiliza kwenye taarifa tayari zoezi hili limeandaliwa vyema katika utunzaji hivyo tutatekeleza ili kuliweka jiji letu katika mazingira bora”amesema Mhe.Maganga
Naye Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa mazingira jiji limejiwekea sheria ndogo zinazowataka wananachi wote wanaomiliki ardhi kupanda miti mitano kwenye maeneo yao pamoja na maeneo ya taasisi za umma ili kuliweka jiji katika mazingira pendezeshi
“Sheria ndogo za utunzaji na usimamizi wa Mazingira za Jiji la Dodoma zimesambazwa katika Kata na Mitaa ili kudhibiti mifugo inayokula miti inayokua na uvamizi wa jamii kwenye misitu ya asili”amesema Kimaro.