Matukio katika mechi ya robo fainali Kati ya Ifuenga United na Young Stars
……………………………………………………………
LIGI soka daraja la tatu mkoa wa Iringa inayojulikana kwa jina la Asas Super League 2020 hatua ya nane bora imeendelea leo katika uwanja Kalenga na kuzikutanisha timu za Ifuenga United na Young Stars.
Katika mchezo huo timu ya Ifuenga Fc ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Young Stars lilofungwa na Joram Ngao katika dk 79 ya mchezo.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali ikichezeshwa vyema na mwamuzi Msafiri Mbugi akisaidiwa na Hashim Mgimba na Rajabu Luvanga Hadi kipindi Cha kwanza kinaisha Hakuna timu iliyofanikiwa kuondoka na goli.
Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya maziwa ya Asas kwa miaka mitatu ilishuhudiwa mechi nyingine katika hatua ya nane bora Kati ya Chuo Cha Iringa na Irole ambapo matokeo ni Chuo Kikuu Cha Iringa 0-2 Irole F.C kwa magoli yaliyofungwa na Christopher kidava dk 25 na Zedi Zedi Dk 86.
Kwa matokeo hayo timu za Ifuenga United na Irole Fc zimefanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano zikiungana na Ivambinungu Fc na Kidamali fc.
Nusu fainali ya kwanza itazikutanisha timu ya Ivambinungu fc na Kidamali fc siku ya Jumapili katika uwanja wa Wambi.
Fainali ya Pili Itakuwa Kati ya Irole fc na Ifuenga United.