Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akimsikiliza Mkuu wa wilaya wa Kongwa Dkt. Suleiman Serera kabla ya kuanza ukaguzi wa maeneo ya barabara yaliyoharibiwa na Mvua wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akiwa na Mkuu wa wilaya wa Kongwa Dkt. Suleiman Serera wakikagua barabara ya Kongwa mjini inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo amemuelekeza Mkandarasi Mtuvilo Traders anayejenga barabara hiyo kufanya marekebisho kwa kuweka makaravati ili kuzuia maji kujaa barabarani na kuingia katika makazi ya watu.
Muonekano wa barabara ya Kongwa mjini inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akizungumza mara baada ya kukagua barabara ya Kongwa mjini inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo amemuelekeza Mkandarasi Mtuvilo Traders anayejenga barabara hiyo kufanya marekebisho ili kuzuia maji kujaa barabarani na kuingia katika makazi ya watu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akimsikiliza Mkuu wa wilaya wa Kongwa Dkt. Suleiman Serera akitoa maelezo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Kongwa mjini.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akiendelea na ukaguzi wa daraja la Chamkoroma linalounganisha wilaya ya Mpwapwa na Kongwa ambapo ametoa siku mbili kwa Mkandarasi kujenga njia ya Mbadala ili kuwawezesha wananchi kupita wakati ujenzi ukiendelea.
Muonekano wa njia ya Mbadala inayojengwa ili kuwawezesha wananchi kupita wakati ujenzi wa daraja la Chamkoroma ikiendelea .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akitoa maelekezo kwa Mkandarasi (hayupo pichani) anayejenga daraja la Chamkoroma linalounganisha wilaya ya Mpwapwa na Kongwa kujenga njia ya Mbadala ili kuwawezesha wananchi kupita wakati ujenzi ukiendelea.
Kaimu Meneja wa TANROADS mhandisi Salome Kabunda,akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Chamkoroma linalounganisha wilaya ya Mpwapwa na Kongwa.
Mkuu wa wilaya wa Kongwa Dkt. Suleiman Serera,akizungumza wakati wa ukaguzi wa maeneo ya barabara yaliyoharibiwa na Mvua wilayani humo.
Diwani wa kata ya Chamkoroma Saimon Binde,akizungumza mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,kukagua ujenzi wa akitoa maelekezo kwa daraja la Chamkoroma linalounganisha wilaya ya Mpwapwa na Kongwa.
Muonekano wa Daraja la Chamkoroma linalounganisha wilaya ya Mpwapwa na Kongwa mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge kufanya ukaguzi wa maeneo ya barabara yaliyoharibiwa na Mvua.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Kongwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ametoa siku mbili kwa Mkandarasi anayejenga daraja la Chamkoroma lililopo wilayani Kongwa kujenga njia ya Mbadala ili kuwawezesha wananchi kupita wakati ujenzi ukiendelea.
Daraja hilo lipo ndani ya barabara ya Pandambili-Mlali -Mpwapwa hadi Ngh’ambi inayojengwa kwa gharama ya Sh Bilioni 1.1 na mkandarasi Bahati Investment.
Kauli hiyo ameitoa January7,2021 wilayani Kongwa katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maeneo yaliyoharibiwa na mvua.
Dkt.Mahenge amesema kuwa daraja hili ni muhimu kwani linaunganisha wilaya ya Mpwapwa na Kongwa ambalo kuharibika kwake kumepelekea uwepo wa changamoto ya usafiri na hivyo kurudisha nyuma uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na halmashauri kwa ujumla.
“Daraja hili ni muhimu sana katika kukuza uchumi wetu,kuharibika kwake kumezuia shughuli za kiuchumi kwa wananchi kuendelea,niwapongeze Wakal wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dodoma kwa usimamizi lakini niwaombe mumsimamie mkandarasi huyu ili akamilishe kwa wakati,,na njia mbadala isizidi siku mbili iwe imekamilika,”amesema Dkt.Mahenge
Dkt Mahenge amewataka TANROADS kumsimamia mkandarasi ili daraja lijengwe kwa kiwango kuendana na thamani ya pesa iliyotolewa na liweze kukamilika kwa muda uliowekwa.
“Wekeni structure ambayo wataalam mtaridhika nayo,unapojenga kitu kisichokuwa na ubora haikudumu na baada ya muda fulani kinaharibika na hivyo kuzuia fedha ambazo zingetumika kwingine,naomba mjiridhishe na kile ambacho kitafanyika hapa ili kiwe Cha uhakika,”amesisitiza Dkt Mahenge.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya wa Kongwa Dkt. Suleiman Serera ,amewakumbusha wananchi suala la upandaji wa miti ili kuzuia wingi wa maji unaoharibu miundombinu ya barabara.
“Hivi karibuni nilifanya kikao hapa na kuhimiza suala la utunzaji wa mazingira Ili kuokoa miundombinu yetu,tukipanda miti kwa wingi maji yanayopita hapa hayatakuja kwa kasi hadi kupelekea uharibifu wa miundombinu,”amesema Dkt Serera.
Awali
amesema kuwa wanachokifanya kwa Sasa ni kuona namna ya kuzuia maji ili yasiweze kuleta uharibifu zaidi wakati huu ambapo kazi inaendelea.
“Kazi hii tunayoifanya ipo kwenye uwezo wa mkandarasi na ndani ya wiki tatu au mwezi mmoja mkandarasi ameahidi kukamilisha daraja hili,na tuahidi kuwa tutamsimamia ili akamilishe kwa wakati,”alisema.
Naye Diwani wa kata ya Chamkoroma Saimon Binde amesema kuwa tatizo lililopo ni uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa na wananchi.
“Hapa Kuna wananchi wamejimilikisha ardhi mlimani huko,wanalima wanafanya uharibifu wa kukata misitu na hivyo kumaliza misitu iliyopo na kupelekea eneo hili kwa kiasi kikubwa kuharibiwa na mvua,”alisema.
Ziara ya Dkt Mahenge ilianzia kwenye kukagua barabara ya Kongwa mjini inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo amemuelekeza mkandarasi Mtuvilo Traders anayejenga barabara hiyo kufanya marekebisho kwa kuweka makaravati ili kuzuia maji kujaa barabarani na kuingia katika makazi ya watu.