********************************************
Na: fadhilakizigo
Simamia misimamo yako hata kama watakupinga wengi ila ni vyema kusimama na unachokiamini kwenye maisha yako usiyumbishwe na matakwa ya watu kwani watakurudisha nyuma kila siku.
Unaweza usiamini hili ila ndio ishatokea Kocha mkuu wa klabu ya Simba Sven Vandebroek tayari amekusanya vilago vyake na kuachana na klabu yake kwa makubaliano ya pande zote mbili taarifa hizi ni za masikitiko makubwa kwa wapenda soka ukizingatia mafanikio yalionekana siku moja kabla ya kuachia ngazi kwa Kocha huyo ni ajabu kusikia taarifa hizi tena ghafla kwa shabiki,mdau wa soka najua umeshitushwa na taarifa hizi za kuachia ngazi kwa kocha Sven licha ya kuwafikisha kwenye group stage kwa ushindi mkubwa wa goli nne.
SVEN ALISTAHILI KUONDOKA SASA?
Binafsi naamini uwezo wake na mafanikio yaliyopatikana kwenye kipindi chake kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara,Ngao ya jamii, Kombe la Azam na kuwafikisha kwenye hatua ya makundi heshima hii ya Simba kwa makombe haya hakustahili kuondoka kwenye kipindi hiki cha furaha kwa wana Simba ni kweli ni kama mgeni aje nyumbani kwako kwa furaha ya kusherehekea sikukuuu au sherehe ya harusi halafu kabla hamjamaliza kufurahia mgeni aondoke akiwa amechukia wewe mwenyeji hautajisikia vizuri kwasababu ulimkaribisha kwa mbwembwe zote na amekusaidia baadhi ya maandalizi yako ya sherehe sherehe inataka kuanza akuage naondoka na akiwa hana furah a huu si uungwana na desturi zetu Wa Tanzania tulivyo na sifa ya ukarimu.
KUNA JAMBO LIMEMSIBU SVEN?
Uongozi umetutaarifu ni makubaliano ya pande zote mbili hivyo tushikilie hapo kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili ila kuna usemi unasema akufukuzae akwambii toka sasa sijajua kama vinaingiliana na hili au laa mimi nawewe tushikilie hili kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.
TUTAMKUMBUKA SVEN?
Ni kweli tutamkumbuka kwa misimamo yake kusimamia anakiamini na makocha wote mjifunze kwa Sven kwani aliamini anachokiamini kama kucheza na mshambuliaji mmoja na imempa mafanikio leo tunaisifu Simba kwa ubora wake ila ni mchango Sven ulioleta mafanikio na kubeba makombe kongole Sven utabakia kwenye historia ya Simba na soka la Tanzania .
Imeandaliwa Na Fadhila Kizigo Kocha Mwandishi 0673854979 Instragram fadhilakizigo19