MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Kichama Ndg. Mohammed Rajab Soud alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mwera kwa ajili ya kuyapokera Matembezi ya Vijana wa UVCCM na kuzungumza nao, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, na (kushoto kwa Mama) Makamu Mwenyekiti wa UVCCM ambae pia ni Waziri wa Vijana Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Mwita Maulid.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera kuhudhuria hafla ya kuyapokea Matembezi ya Vijana wa UVCCM, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar na (kulia kwake) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Bi. Hamida Mussa Khamis, wakielekea katika sehemu ilioandaliwa kwa ajili ya hafla hiyo katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera.
NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Mussa Haji Mussa akizungumza na kutowa maelezo ya Matembezi hayo ya Vijana wa UVCCM, kwa mgeni rasmin Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) kabla ya kumkaribisha kuzungumza katika hafla hiyo ya mapokezi ya matembezi hayo iliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera
VIJANA wa UVCCM wanaoshiriki Matembezi ya kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishangilia wakati Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Vijana hao wakati wa mapokezi hayo yaliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM ambae pia ni Waziri wa Vijana Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Mwita Maulid,m akizungumza na Vijana wanaoshiriki Matembezi ya kuadhimisha sherehe za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakati wa hafla ya mapokezi matembezi hayo katika Wilaya ya Magharibi “B” Unguja katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akizungumza na Vijana wanaoshiriki Matembezi ya Maadhimisho ya sherehe za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakati wa hafla ya mapokezi ya Vijana hao katika Wilaya ya Magharibi “B” Unguja katika Skuli ya Msingi Mwera.
VIJANA wa UVCCM wanaoshiriki Matembezi ya kuadhimisha sherehe za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Vijana hao wakati wa mapokezi ya matembezi hayo katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakiwa katika matembezi hayo.
Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Mwalim Kombo Hassan Juma.akizungumza wakati wa hafla hiyo ya mapokezi ya Matembezi ya Vijana wa UVCCM, kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo ya mapokezi imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera.(Picha na Ikulu)