Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Deogratias Manyama akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzilaa mara baada ya kupokea zawadi hizo Mbunge wa jimbo la Kibamba Mhe. Issa Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi na waandishi wa habari mara baada ya kuwapatia zawadi wagonjwa hospitalini hapa.
Mhe.Issa Mtemvu akimkabidi Bw. Zablon Mchagula zawadi wakati alipotembelea wodi ya wanaume hospitalini hapa (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji Dkt. Manyama.Mtemvu akimpa pole Bw.Abduly Rashid alipokuja kutembelea wagonjwa Mloganzila.
************************************************
Mbunge wa jimbo la Kibamba Mhe.Issa Mtemvu amewatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kutoa zawadi kwa baadhi ya wagonjwa wenye uhitaji .
Zawadi hizo zimejuisha pampasi za watu wazima, mafuta ya nazi,Maji ya kunywa,sabuni,miswaki pamoja na dawa ya meno
Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Deogratias Manyama amemshukuru mbunge huyo kwa kuwatembelea wagonjwa na kutumia fursa hiyo kueleza baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali ikiwemo gharama za uendeshaji pamoja na changamoto ya vyombo vya usafiri.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi katika wodi ya wagonjwa wenye uhitaji hospitalini hapa, Mhe. Issa Mtemvu amesema kuwa lengo la kutembelea Mloganzila ni kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa na kuwatakia heri ya mwaka mpya.
“Nimekuja kuwapa mkono pole kama mwakilishi wenu bungeni na kuwatakia heri ya mwaka mpya pamoja na kutumia fursa hii kusikiliza changamoto zinazoikabili hospitali hii ili niweze kuziwasilisha bungeni kwa waziri mwenye dhamana”amesema Mhe. Mtemvu
Mhe. Mtemvu amewataka wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa uhakika.