*******************************************
NJOMBE
Kufuatia mkoa wa Njombe kutegemea mapato yake mengi mashambani na misituni,wajumbe wa kiako cha bodi ya barabara mkoa wa Njombe wamejikuta katika mgongano wa hoja kuhusu kuzia magari makubwa yanayozidi tani 10 kuingia katika maeneo muhimu ya uzalishaji ili kunusuru uharibifu mkubwa wa barabara unatokea mapema baada ya matengenezo.
Mkoa wa Njombe unazalishaji kiasi kikubwa cha mazao ya biashara na chakula kama vile Viazi,Chai,Mbao na parachichi jambo ambalo linawalazimu wafanyabiashara kutumia magari makubwa kufata malighafi kwa wakulima na kusababisha uhalibifu mkubwa wa barabara.
Agnetha Mpangile,Edwin Swale mbunge wa Lupembe na Joseph Kamonga mbunge wa Ludewa wakitoa uchauri kuhusu namna ya kumaliza changamoto hiyo bila kumuathiri mfanyabishara na mkulima wamesema kuweka zuio hilo itakuwa tatizo kubwa kwa mkulima na kwamba kinachotakiwa kuiongezea bajeti TARURA na TANROADS ili ijenge barabara kwa kiwango cha changarawe ama lami ili kukidhi mahitaji ya uchumi uliopo.
Akifafanua kwanini TARURA imekuwa ikizidiwa mhandisi mwandamizi wizara ya ujenzi Clemence amesema wakala huo umekuwa ukifanya kazi ya ujenzi wa barabara nyingi na ambazo zipo nje mtandao wake huku kaimu meneja wa TANROAD mkoa wa Njombe mhandisi Ruth Shalluah akibainisha hatua zinazochukuliwa ili kuboresha mtandao wa barabara Njombe kwa kuendelea na usafiri na ukarabati katika maeneo mengi.
Baada ya mgongano wa muda mrefu ndipo mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akatoa ushauri wake kwamba tuendelee kutafuta mizani ya kupima uzito huku barabara zikiendelea kuboreshwa kwa manufaa ya watu..
Kwa Mujibu wa takwimu za TANROAD Mkoa wa Njombe una mtandao wa barabara wenye urefu wa 1200.885 km