Home Mchanganyiko PROF.KABUDI AONGOZA JOPO LA MAWAZIRI SITA KUFANYA ZIARA YA UKAGUZI MAENEO AMBAYO...

PROF.KABUDI AONGOZA JOPO LA MAWAZIRI SITA KUFANYA ZIARA YA UKAGUZI MAENEO AMBAYO ATATEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA

0

****************************************************

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameongoza jopo la mawaziri sita kufanya ziara ya kukagua maeneo ambayo Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Wang Yi atatembelea wakati wa ziara yake hapa nchini na kuonesha kuridhishwa na mazingira hayo. Mawaziri hao wametembelea, Uwanja wa ndege wa Geita-Chato, Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) na Mwalo wa Chato.

Prof. Kabudi ameambatana na mawaziri wenzake ambao ni pamoja na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Jumanne Kishimba wakiwa wameambatana na Makatibu Wakuu wa wizara hizo.