WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,Dk Faustine Ndugulile akizungumza leo 6.1.2021 jijini Dodoma baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kuzungumza na watendaji,wafanyakazi ,Menejimenti na wajumbe wa bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF).
Baadhi ya watendaji wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,Dk Faustine Ndugulile alipofanya ziara ya kutembelea na kuzungumza na watendaji,wafanyakazi ,Menejimenti na wajumbe wa bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) leo 6.1.2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , Dk Zainab Chaula akizungumza na watendaji,wafanyakazi ,Menejimenti na wajumbe wa bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) leo 6.1.2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu UCSAF, Justina Mashiba,akimshukuru Waziri wa kuwatembelea huku akisema maelekezo yote wamejipanga kuyafanyia kazi leo 6.1.2021 jijini Dodoma.
Afisa Fedha Mkuu USCAF Bi.Josephine Mathee,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyakazi wenzake kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,Dk Faustine Ndugulile ambaye alifanya ziara ya kutembelea na kuzungumza na watendaji,wafanyakazi ,Menejimenti na wajumbe wa bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) leo 6.1.2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amewataka watendaji wa wizara hiyo kuangalia mapungufu ya kisheria yaliyopo yanayokwamisha utendaji kazi katika baadhi ya maeneo ili ziweze kufanyiwa marekebisho na kutoa majibu ya changamoto zilizopo.
Aidha amesema kuwa anataka kuona Tanzania ijiendeshe kidigitali na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano itumike vyema kwa kuweka mifumo mizuri ili kuisaidia serikali kujiendesha na kuongeza mapato katika kukuza uchumi.
Kauli hiyo ameitoa leo 6.1.2021 mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kuzungumza na watendaji,wafanyakazi ,Menejimenti na wajumbe wa bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) jijini Dodoma
Aidha Dk.Ndugulile amesema kuwa hataki kusikia kisingizio vya mapungufu ya kisheria katika kukwamisha baadhi ya utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo waache kufanya kazi kwa mazoea waende mbali zaidi.
“Kaeni muainishe mapungufu ya kisheria mnayoona yanawakwamisha katika kupeleka mawasiliano kwa watanzania, sheria sio msahafu, kanuni pia vyote vinaweza kurekebishwa,” amesisitiza Dk.Ndugulile
Hata hivyo Dk.Ndugulile amesema kuwa mpaka sasa zaidi ya watanzania milioni 12.2 wamefikiwa na huduma ya mawasiliano huku kata 361 nchini zikiwa hazijafikiwa, zikiwekwa kwenye mpango wa kukamilika katika miaka mitano iliyopo.
Ameitaka UCSAF kuangalia namna ya kupunguza gharama za minara ili waweze kupeleka mawasiliano kwa watanzania na kqa gharama nafuu.
Aidha amesema kuwa hakubaliani na Takwimu zilizotolewa na wataalam kuwa inachangia kwa asilimia 0.5 kwenye mapato serikali
“Mchango wa TEHAMA ni mkubwa na kuna mambo makubwa yanayofanywa kupitia Teknolojia hiyo mnaposema inachangia mapato kwa asilimi 0.5 sitaki kukubaliana nayo, najua ni zaidi ya hapo na ninataka ijiendesha mpaka kufikia kiasi Cha kuchangia mapato kwa asilimia 10, kaeni mpitie upya Takwimu zenu,”amesema Dk.Ndugulile.
Naye Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba, amesema kuwa wamepokea maelekezo yote ya waziri na wamejipanga kuhakikisha wanatoka katika kufanya kazi kwa mazoea na kutumia ushauri na maelekezo aliyoyawapatia ili kupiga hatua zaidi na ziweze kuendana na wakati wa sasa kwa upande wa TEHAMA.
Bi.Mashiba amesema kuwa Januari 22 wamepanga kufanya kikao na watoa huduma za mawasiliano nchini katika suala zima la kujipanga ili waweze kupeleka huduma ya inteneti ya 3G katika maeneo ya pembezoni kama waziri alivyoagiza ambapo awali wao walikuwa wakipeleka huduma hiyo kwa kutumia 2G.
Bi.Mashiba amesema kuwa mapungufu ya huduma za minara katika kupeleka mawasiliano kwa wananchi watahakikisha wanatumia gharama nafuu za kupeleka huduma hiyo waweze kuwapatia watanzania huduma ya mawasiliano kwa gharama nafuu.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Afisa Fedha Mkuu UCSAF Bi.Josephine Mathee amesema kwa wamepokea maagizo yote ya waziri na sasa wanaenda kutekeleza kwa vitendo.