Watoto wa Marehemu Rosemary Nyerere wakiwa wamebeba shada la maua wakati wa Mazishi ya mama yao yaliyofanyika katika makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika kituo cha Hija Pugu Jijini Dar es salaam, Januari 6, 2021
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwe udongo katika kaburi la Rosemary Nyerere ambaye ni Mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambara Nyerere katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika Kituo cha Hija Pugu Jijini Dar es Salaam, Januari 6, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiweka shada la maua katika kaburi la Rosemary Nyerere ambaye ni Mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambara Nyerere katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika Kituo cha Hija Pugu Jijini Dar es Salaam, Januari 6, 2021. .
Wawakilishi wa Mkoa wa Mara wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wakiweka shada la maua katika kaburi la Rosemary Nyerere ambaye ni Mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambara Nyerere katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika Kituo cha Hija Pugu Jijini Dar es Salaam, Januari 6, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole Makongoro Nyerere (Katikati) na Anna Nyerere (Kushoto), wakati aliposhiriki mazishi ya Rosemary Nyerere ambaye ni Mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambara Nyerere katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika Kituo cha Hija Pugu Jijini Dar es Salaam, Januari 6, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki mazishi ya mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rosemary Nyerere aliyefariki dunia Januari Mosi, 2021.
Mazishi hayo ya Rosemary Nyerere yamefanyika leo (Jumatano, Januari 6, 2021) katika makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo kwenye Kituo cha Hija kilichoko Pugu jijini Dar es Salaam.
Ibada ya mazishi imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Upanga jijini Dar es Salaam, Dias Mario.
Viongozi wengine walioshiriki katika mazishi hayo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba.
Wengine ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula.
Viongozi wengine ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi, Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakary Kunenge na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima