Na Ahmed Mahmoud Arusha
Kijana mwenye umri wa miaka 27 aliyenufaika na mitandao ya kijamii amewajengea wazazi wake nyumba ya milioni 137 kama zawadi kwao baada ya kupata fedha hizo na kuweka heshima kijijini kwao.
Aidha wananchi wengi wanaudharau umri wangu Mdogo wa miaka 27 kwa mambo makubwa niliyo Fanya kwa muda wa miaka 2 baada ya kunufaika na fedha nilizopata. baada kuwajengea wazazi wake nyumba kijijini Magadirisho iliopo usa river wilayani Arumeru mkoani Arusha
Akizungumza na vyombo vya habari @Masipety ameleza kwamba taaluma yake ni ufamasia aliyosoma kwa muda wa mika minne lakini aliamua kuacha na kujikita katika kufanya kazi katika mitandao ya kijamii ikiwemo instergram pamoja na mtandao wa Facebook akilenga kutumia taaluma yake ya ufamasia kuwafikia vijana na kina mama
Amesema mpaka sasa ameishawasaidia vijana zaidi ya 50 kupata ajira kupitia mitandao na kutaka vijana kuacha kulalamika hakuna ajira wakati wanaitumia mitandao ya kijamii vibaya kutukana viongozi na kuendesha siasa au kutumia kwa mambo mengine yasiojenga jamii.
Masipety ameeleza kwamba watu wengi wamekuwa wakitumia mitandao vibaya badala ya kujinufaisha kwa kutangaza biashara zao au kile kipaji alichopewa na Mungu kutumia kujiongezea kipato
Amebainisha kwamba mpaka sasa amefanikiwa kujenga nyumba ya kuishi yenye gharama ya shilingi Million 200 katika eneo la Njiro lililopo jiji la Arusha na anamiliki viwanja vingine Dar es salam huku akiendelea kusaidia wanawake katika masuala ya afya .
@masipety amesema kwa siku anauwezo wa kuingiza kiasi cha million 1 kwani taaluma yake imekuwa ikiwagusa kina mama wenye matatizo ya afya hasa matatizo ya uzazi hivyo kupitia taaluma ya ufamasia imekuwa chachu ya maendeleo makubwa kwake na familia yake.
“Ndugu zangu waandishi kusema ukweli mtandao umenipa heshima kubwa sana mpaka kufikia kuacha kazi ya ufamasia na kufanya kazi ya kuelimisha jamii na kuwahudumia kinamama kutatua changamoto za uzazi jambo ambalo limekuwa ni tatizo sugu kwao pia nimewaajiri vijana zaidi ya 50 kupitia taaluma ya ufamasia kutumia fursa ya mtandao kujiongezea kipato” alisema @masipety
Kwa upande wake mama mzazi wa Masipety Bibi Stela Mmasi ameshukuru kwa mafanikio makubwa aliyopata kwa muda mfupi wa miaka miwili huku akisema kuona msichana wa kike anakumbuka wazazi ni jambo la baraka sana hakutegemea kuona akiwafanyia mabadiliko ya maisha waliokuwa wakiishi mwanzo.
Stela amesema mpaka sasa mwanae huyo amewasaidia kuinua familia yao katika kuwasomesha ndugu zake Jamaa wa kijijini kwao na hata yeye @masipety alihadi endapo atafanikiwa kumaliza masomo yake angeisaidia jamii isiyo kuwa na uwezo kupata elimu au kupata ajira
Hata hivyo binti Masipety ametoa rai kwa vijana kumfuatilia katika mitandao yake ya kijamii kwa kuwasaidia zaidi kupata ajira na kuwasomesha wale ambao hawana uwezo kutosita kuusogelea msaada huo.