Meneja Huduma za kadi wa Benki ya NMB, Ednamamu Shobi akichezesha droo ya tano ya Promosheni ya NMB MASTABATA jijini Dar es Salaam. katikati ni Meneja Mwandamizi Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Lupia Matta na kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Joram MatafyaMeneja Huduma za kadi wa Benki ya NMB, Ednamamu Shobi akizungumza wakati wa kuchezesha Droo ya tano ya Promosheni ya NMB MASTABATA jijini Dar es Salaam. katikati ni Meneja Mwandamizi Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Lupia Matta na kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Joram Matafya
***************************************************
NA MWANDISHI WETU
BENKI ya NMB, tayari imeshatumia jumla ya shilingi milioni 20 kwaajili ya washindi 200 wa droo za wiki tano tangu kuanza kwa promosheni ya NMB Mastabata mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.
Leo benki hiyo ilitangaza washindi 40 wa droo ya 5 ya Kampeni ya NMB MastaBATA, idadi inayofanya jumla ya washindi 200 hadi sasa kuwa wamejishindia Sh. 100,000 kila mmoja kati ya washindi 400 wanaotarajiwa kuzawadiwa katika kipindi cha kampeni hiyo.
NMB MastaBATA, ni Kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24, 2020 na itadumu hadi Februari 2021, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo pesa, simu janja, jokofu, runinga na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.
Akizungumza wakati wa Droo ya wiki ya tano iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi wa NMB, Lupia Matta, alisema kampeni hiyo imeongeza idadi ya watumiaji wapya wa Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR kwa asilimia 50.
Matta alibainisha kuwa, NMB MastaBATA na NMB Friyay, kampeni mbili zinazochagiza matumizi ya NMB Mastercard na Mastercard QR, zimeonesha mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya watumiaji kwa asilimia 50.
“Kumekuwa na zaidi ya asilimia 50 ya watumiaji wapya wanaoingia katika utamaduni wa manunuzi kwa kutumia kadi, idadi ambayo imeongezeka katika kipindi hiki cha kuanzia Julai 2020 hadi sasa.
“Tuna kampeni mbalimbalii za kuchagiza matumizi ya Mastercard na Mastercard QR, kabla ya MastaBATA tulikuwa na NMB Friyay, inayotoa punguzo la asilimia 15 ya bei za manunuzi kupitia kwa wauzaji ambao ni wabia wetu kibiashara kote nchini,” alifafanua Matta.
Washindi 40 waliopatikana katika droo ya Januari 5, wanafanya idadi ya washindi waliojinyakulia Sh. 100,000 kufikia 200, ambayo ni nusu ya washindi (400) watakaopatikana katika kampeni hiyo hadi Februari itakapofikia tamati.
Matta aliwataka wateja wa NMB wanaotumia Mastercard na Mastercard QR, kuendelea kufanya manunuzi ya bidhaa na malipo mengine, ili kujiongezea nafasi za kushinda zawadi mbalimbali, ikiwamo ya Grande Finale ya kufanya utalii wa ndani Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti.
Aidha, washindi watakua na uhuru wa kuchagua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu, Laptop, Simu (Samsung A70), Water Dispenser na Microwave.
Pia, Matta alisema kuwa NMB MastaBATA itawazawadia washindi 15 simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Shilingi Mil. 2.4 kila mwezi, ambako aliwataka wateja wa NMB kuchangamkia zawadi hizo nono.
Droo ya 5 ya NMB MastaBATA, imefanyika chini ya uangalizi wa Joram Mtafya, Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), aliyetoa wito kwa wateja wa NMB kutokuwa na shaka na mchakato unaozalisha washindi wa kampeni hiyo.