***************************************************
NJOMBE
Baada ya kubaini kwamba barabara ya TANZAM iliyojengwa 1968 kutoka Dar es salaamu hadi Lusaka Zambia inatumiwa sana katika biashara chafu ya usafirishaji wa wahamiaji haramu kwenda africa ya kusini kwasababu mbalimbali zikiwepo za kimaisha na usalama,Vikosi vya uhamiaji mkoani Njombe vimeongeza ulinzi ili kudhibiti uhalifu huo unaodaiwa kufanywa na mtandao wa watu wakigeni na watanzania.
Barabara kuu ya TANZAM ni kiunganishi kikuu cha mataifa ya africa mashariki na kati huku ikitumika sana kibishara na nchi za Zambia, Marawi,Rwanda,Burundi,Congo,Kenya na Africa ya Kusini, jambo ambalo limekuwa likisababisha watanzania wasio wazalendo kutumia mwanya huo kufanya biashara chafu na magendo.
Kutokana na hali hiyo vikosi vya jeshi la uhamiaji mkoa wa Njombe vimelazimika kuongeza nguvu katika kituo kidogo cha Makambako kwa kufanya patro masaa 24 na nyakati za mvua kali ambazo zinatajwa kuwa ndiyo nyakati zinazotumika sana na watanzania wasio wazalendo na mitandao yao kuvusha magendo na wahamia haramu,Kama ambavyo mkuu wa uhamiaji mkoa kamishna Msaidizi John Yindi anavyoeleza kwamba watafanya operesheni za siri na wazi kubaini watanzania wanaohusika na mtandao wao
Mara baada ya vikosi vya uahamiaji kumefanya operesheni kali ya ukaguzi wa magari ya abiria,mizigo,bajaji na bodaboda ili kunasa wahamiaji haramu usiku wa kuamkia leo ndipo Madereva wakatoa maoni yao kwamba watafichua viashiria vyovyote vya kialifu katika Njia kuu ya Inayopita mjini Makambako
Kabla ya kufanya operesheni hiyo lilifanyika zoezi la uzinduzi wa ofisi ya mkuu wa kituo cha uhamiaji Makambako likihudhuriwa na mwenyekiti wa mtaa wa Mizani Kervin Mwagili ambaye ana ahidi kushirikina kuwanasa wahalifu.