Home Michezo MATI SUPER BRANDS YAKARIBISHA MWAKA 2021 KWA BONANZA

MATI SUPER BRANDS YAKARIBISHA MWAKA 2021 KWA BONANZA

0

Mkurugenzi wa Mati Super Brands David Mulokozi akizungumza na wafanyakazi wa kampuni yake kwenye bonanza la kufurahia maliza kwa mafanikio mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka 2021.

Wafanyakazi wa kampuni ya Mati Super Brands Ltd na Mkurugenzi wao David Mulokozi wakiwa kwenye bonanza hilo.

Wafanyakazi wa kampuni ya Mati Super Brands Ltd wakimsikiliza Mkurugenzi wao David Mulokozi kwenye bonanza hilo.

************************************************

Na Mwandishi wetu, Babati

KATIKA kuhitimsha mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2021 kampuni ya Mati Super Brands chini ya mkurugenzi wake David Damian Mulokozi wamefanya bonanza kubwa la kufunga mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2021.

Viongozi pamoja na wafanyakazi wote wa Mati Super Brands kutoka maeneo tofauti ya nchi walikutana na kushiriki michezo mbalimbali katika uwanja wa Singe Mjini Babati Mkoani Manyara.

Hata hivyo Mkurugenzi ndugu David Mulokozi amesema lengo la bonanza hilo ni kudumisha umoja na ushirikiano miongoni mwao kuanza mwaka 2021.

Pamoja na hayo wafanyakazi wa Mati wameushukuru uongozi wa Mati kwa kuwajali sana na kuahidi kufanya kazi katika misingi imara zaidi mwaka 2021.

Katika baadhi ya michezo ikiwemo WAR walishinda team Strong dry gin, Mpira wa miguu walishinda team Strong Coffee, Kukimbiza kuku upande wa wanaume alishinda mfanyakazi wa kitengo cha Masoko Kusiri, upande wa wanawake alishinda Meneja burudani wa The Champions lounge Teddy, Dancing competition alishinda mfanyakazi wa kitengo cha Production Mashine, katika sanaa na ubunifu walishinda team strong dry gin ndani yake akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa Mati Super brands ltd David Mulokozi na shindano la kula alishinda mfanyakazi katika kitengo cha masoko na mauzo Mkoani Tanga, Mathias Masele.