*******************************************
Kuna mda inabidi tujifunze kujali vya kwetu kwani ni moja ya uzalendo wa kukubali na kuthamini vya kwetu na sio vya wenzetu.
Zikiwa zimesalia siku tatu kuelekea kwenye mchezo wa marudiano ya klabu bingwa barani Afrika kati ya Simba dhidi ya Fc Platnum ya nchini Zimbabwe huku mchezo huo ukiwa na taswira kubwa kwani atakayepoteza mchezo huo atakuwa ametolewa kwenye mashindano hayo na kwenda kwenye shirikisho moja kwa moja ikumbukwe ya kwamba mchezo wa awali Simba alipoteza akiwa ugenini nchini Zimbabwe kwa goli moja pekee lililofungwa na Chikwende perfect hivyo Fc Platinum wanakuja Daressalaam kwa Mkapa wakiwa na goli moja walililofunga wakiwa nyumbani na atakayeshinda mchezo huo atakuwa amevuka hatua iyo na kwenda kwenye hatua ya makundi.
Namuona Sven akifunguka zaidi kwenye mchezo huu dhidi ya Fc Platnum kwa Mkapa kwani hawana cha kupoteza wanahitaji magoli mawili na zaidi ili kuwahakikishia kuendelea kusalia kwenye mashindano na kwenda hatua nyingine ya makundi ukifunguka zaidi unahitaji pia kuwa bora zaidi kwenye safu yako ya ulinzi kwani nataraji kuwaona Fc Platinum wakijilinda zaidi ili kulinda goli lao na kufanya mashambulizi ya kustukiza counter attack na kwa aina ya makosa ya safu ya ulinzi ya Simba kwenye mechi ya awali kule Zimbabwe walinzi wake walifanya makosa ambayo yaliwaadhibu kwa goli walilofungwa na kwa aina ya washambuliaji wa Fc Platinum wanakasi wakiwa wanashambulia inayomlazimu mlinzi kufanya makosa na kujikuta tayari ashakosea kwenye eneo la hatari pengine kasi ya washambuliaji wa Fc Platinum ndio iliwagharimu zaidi walinzi wa Simba kwenye mchezo wa awali kule Zimbabwe sitarajii kuona makosa yakijirudia tena kwenye ardhi ya nyumbani kwa Mkapa.
Wachezaji wanaweza kuamua matokeo wakiwa uwanjani kwa walichofundishwa na kocha lakini kocha anazoasilimia kubwa za kuamua matokeo kwa kubadilika kutokana na aina ya wapinzani wako kwa dk 15 za awali kocha Sven ndio muamuzi mkubwa wa mchezo huu dhidi ya Fc Platnum na wachezaji wanaamua kutokana na waliyofundishwa na kocha kwa kuzingatia sychology ya wachezaji.
Imeandaliwa Na: Fadhila Kizigo Kocha Mwandishi 0673854979 Instragram fadhilakizigo19