Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) amesherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021 kwa kuwatembelea na kuwapatia zawadi watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.
Mhe. Katambi ametembelea watoto hao leo Ijumaa Januari 1, 2021 akiambatana na Katibu wa Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mkama Nyamwesa, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam na Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini, Raphael Nyandi.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa na Mhe. Katambi kwa watoto ni pamoja na unga wa ngano, sukari, madaftari, kalamu,chumvi, sabuni na juisi huku akiwapa motisha walimu walezi wa watoto hao.
Akizungumza, Katambi amesema lengo la ziara yake katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija ni kuwapa salamu za Mwaka Mpya 2021 kutoka kwa viongozi Wakuu wa nchi wakiongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
“Lengo la mimi kufika hapa ni kuwapa watoto salamu za Mwaka mpya 2021 za Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa”, amesema Katambi.
Amesema lengo jingine ni kufuatilia maendeleo ya kituo cha kulelea watoto cha Buhangija, kutatua changamoto za kituo hicho na kuwapa watoto zawadi mbalimbali za Mwaka Mpya 2021 na kuwapa motisha walimu walezi wa wanafunzi hao.
Mhe. Katambi amebainisha kuwa Serikali inatoa kipaumbele na kuyajali makundi maalumu ya watu (wenye uhitaji maalumu) katika jamii wakiwemo watoto wenye ulemavu, wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Katika hatua nyingine, Katambi ametoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla wajitokeze kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji kama vile mafuta maalumu kwa ajili ya watoto wenye ualbino, nguo na chakula akidai kuwa hiyo ndiyo Sadaka, Sala na Dua ya kweli kwa Mungu yenye majibu ya neema.
Mmoja wa watoto hao kwa niaba ya wenzake, Kwandu Masunga amemshukuru Mhe. Katambi kwa kusherehekea nao Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021 na kuwaomba wadau wengine kutembelea kituo hicho kwani wanafarijika na kufurahi wanapopata wageni.
Kwa upande wake, Mkuu wa kituo cha Kulelea watoto cha Buhangija, Mwalimu Suleiman Kipanya amesema kituo hicho sasa kina jumla ya watoto 225 ambapo kati yao wenye ualbino ni 131, wasiosikia (viziwi) 74 na wasioona 20.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Mjini Shinyanga leo Ijumaa Januari Mosi ,2020 kwa ajili ya kuwapa zawadi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam, mtoto Kwandu Masunga na Katibu wa Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mkama Nyamwesa. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa kituo cha Buhangija, Selemani Kipanya. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Mjini Shinyanga leo Ijumaa Januari Mosi ,2020 kwa ajili ya kuwapa zawadi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021.
Mtoto Kwandu Masunga akimshukuru Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) kwa kutembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Mjini Shinyanga leo Ijumaa Januari Mosi ,2020 na kuwapa zawadi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021.
Muonekano wa sehemu ya zawadi za Mwaka Mpya 2021 zilizotolewa na Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) leo Ijumaa Januari Mosi ,2020 kwa ajili ya watoto katika kituo cha Buhangija ili kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021.
Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa kituo cha Buhangija Selemani Kipanya. Wa kwanza kulia ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Raphael Nyandi akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Mukadam.
Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa kituo cha Buhangija Selemani Kipanya. Wa kwanza kulia ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Raphael Nyandi akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Mukadam.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) na msafara wake akipiga picha ya kumbukumbu na watoto na walimu katika kituo cha Buhangija.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) na msafara wake akipiga picha ya kumbukumbu na watoto na walimu katika kituo cha Buhangija.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akipiga stori na mmoja wa watoto katika kituo cha Buhangija huku amembeba wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021 leo Januari 1,2021.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog