Home Michezo SUPER D BOXING PROMOTIOBN KUMRUDISHA HAMISI MAYA ULINGONI APRIL 2

SUPER D BOXING PROMOTIOBN KUMRUDISHA HAMISI MAYA ULINGONI APRIL 2

0

*******************************************

NA MWANDISHI WETU

BONDIA HAMISI MAYA sasa kupanda ulingoni rasmi April 2 katika ukumbi wa Sabasaba Hall uliopo katika viwanja vya Sabasaba akimvaa bondia Alvin Omondi wa Kenya mpambano wa Raundi 8 utakaopigwa katika uzito wa KG 66

Akizungumza kuusu mpambano uho Mratibu wa pambano hilo Chaurembo Palasa amesema kuwa baada ya muda mrefu kukaa kimya kwa bondia huyo sasa anaibuliwa upya na kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion ambao ndio waandaaji wa mpambano uho kwa sasa

Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani ambapo mpaka sasa anasifika kwa kuwapiga mabondia mbalimbali akiwa nje ya nchi ambapo alishawai kumpiga K,O mbaya sana Jems Onyango wa Kenya mpambano uliofanyika Charter Hall, Nairobi  Kenya na kurudi na ubingwa wa Afrika na kumgalagaza bila ya huruma bondia Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kuruni na mkanda

Alisema Palasa ata hivyo mapromota wengi wamekuwa wakimkwepa Maya kutokana na uchezaji wake awapo ulingoni ni kama bondia aliyekusudia kuuwa mtu akiwa mchezoni ndio mana ajapata mapambano tangu mwaka 2019 hata hivyo kupitia kampuni yetu ya Super D Promotion tunampa nafasi ya kuonesha Kipaji chake kwa mara nyingine kwa mwaka uhu 2021

aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho pia kutakuwa na mapambano mengine ya lkukata na shoka ambapo bondia machachali awapo ulingoni Vicent Mbilinyi atazipiga na George Onyango na Fransic Miyeyusho atazipiga na Gabriel Chola wakati Hamidu Kwata atazidunda na Jems Kibazange na juma Abdul wataoneshana kazi na Hamza Mchanjo na Bakari Magona atazipiga na Emanuel Mwakyembe