Home Mchanganyiko NCAA YAJIPANGA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI ILI KUKUZA UTALII NA...

NCAA YAJIPANGA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI ILI KUKUZA UTALII NA UCHUMI

0

   

Kamishhina Msaidizi Mwandamizi wa Mipango na Uwekezaji Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Mhandisi Needpeace Wambuya akitoa mada kwa wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakati walipotembelea makubusho ya Zamadam yaliyopo oneo la Oldupai kwenye hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Baadhi ya picha zikionesha  wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakifuatilia mada ya uwekezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Kamishhina Msaidizi Mwandamizi wa Mipango na Uwekezaji Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Mhandisi Needpeace Wambuya

Baadhi  picha zikionesha wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakifuatilia mada ya uwekezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Kamishhina Msaidizi Mwandamizi wa Mipango na Uwekezaji Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Mhandisi Needpeace Wambuya

Baadhi ya wananchi waoishi katika hifadhi ya Ngorongoro na kuendesha shughuli zaiibinadamu wakiwa katika moja ya eneo la Seneto katika boma lililosheheni tamaduni na mila za jamii zinazoishi katika hifahi ya Ngorongoro.

Baadhi ya wanyama aina ya Pundamilia na mifugo aina ya Gombe inayofugwa na wafugaji katika hifadhi hiyo ikiwa katika bwawa  la Malanja lililopo eneo la Seneto kwa ajili ya kupata kubwa maji.

Hili ndilomeneola Oldupai mahali ambapo panapatikana nyaoza binadamu wa kwanza Zamadam na wanyama lwaioishi miaka mamilioni katika eneo hilo.

Hizi ndizo nyao za Zamadam zilizohifadhiwa katika makumbusho ya Oldupai.

Picha mbalimbali zikionesha wanyama aina ya Nyati, Pundamilia na Simba katika eneo la Ngorongoro Crater ambalo wanyama wa aina mbalimbali hupatikana.

…………………………………..

Kamishhina Msaidizi Mwandamizi wa Mipango na Uwekezaji Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Mhandisi Needpeace Wambuya, amesema  Mamlaka hiyo hivi sasa itajikita katika uwekezaji ili kuchochea maboresho ya sekta ya uhifadhi nchini na kuimarisha uchumi,”alisema.

” Sekta ya utalii ni mtambuka na ina mchango mkubwa katika uchumi hivyo inahitaji mikakati ya pamoja katika uwekezaji.,”alisema.

Aidha alieleza namna walivyojikita katika kufanya uwekezaji ndani ya hifadhi hiyo ili kulinda hadhi ya NCAA na kuboresha changamoto zilizopo, kwa lengo la kuhakikisha hifadhi inaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuchangia pato la Taifa.

“Sifa za NCAA katika ukanda wa Afrika ni za kipekee, hivyo wanahabari na wadau wengine tushirikiane katika kuhakikisha tunalinda maslahi ya hifadhi hii muhimu na kutumia taaluma zetu kuchochea ongezeko la watalii kutoka mataifa mbalimbali,”alisema.

Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 malengo ya serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 idadi ya watalii inaongezeka kutoka Milioni 2 waliopo hadi kufikia Milioni 5 hivyo kuchochea pato la Taifa kukua kwa  Dola za Marekani Bilioni 6.

Wambuya alieleza namna hifadhi hiyo itakavyojikita katika uwekezaji kwa kuzingatia matakwa ya Ilani ya CCM.

Alitaja maeneo ya ndani ya hifadhi yaliyofanyiwa tathimini na kuruhusu uwekezaji, kuwa ni pamoja eneo la mapango lijulikanalo kama Orkarian Gorge, eneo la Mlima wa Lemuta, eneo la Kakese lenye vivutio vingi, na eneo la Oldoinyo Gol ambapo ni karibu na njia ya Nyumba wenye sifa ya kuhama kutoka hifadhini humo kwenda hifadhi ya Serengeti hadi Masai Mara nchini Kenya.

Alisema katika uwekezaji huo wamefungua milango kwa NCAA na sekta binafsi katika maeneo muhimu, yakiwemo ya ndani ya hifadhi kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

Aidha alisema Mamlaka inastawisha uwekezaji kwa lengo la kuongeza vivutio vilivyopo huku ikizingatia hadhi yake na uhifadhi.

” Hatuwezi kuruhusu hujuma na kuharibu mazingira ya hifadhi, hivyo wanaotaka kuwekeza milango iko wazi hususani sekta binafsi tutashirikiana nao ipasavyo lakini hatutaruhusu mahitaji ya uwekezaji yenye kuharibu hali halisi iliyopita,” alisema.

Alisisitiza mpango wa kuruhusu maeneo ya uwekezaji yaliyopo ndani ya hifadhi pia umezingatia GNP ambayo imefanyiwa upembuzi wa kisayansi ili kutokuharibu mazingira ya hifadhini, kwa lengo la kuifanya NCAA kuendelea kuwa na sifa ya hifadhi bora duniani na Afrika.

Alisema uwekezaji katika hifadhi hiyo utasababisha kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka laki 6 kwa Mwaka hadi kufikia Laki 9 mwaka 2025.

” Mtu yeyote atakayepata fursa ya uwekezaji atapata faida kwakuwa hakuna shaka eneo hili ni la kipekee na kumekuwa na vivutio vingi vya utalii,”alisema.