**************************************************
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA LIMEJIPANGA VYEMA KUHAKIKISHA SIKUKUU YA MWAKA MPYA INASHEHEREKEWA KWA AMANI NA UTULIVU.
HATA HIVYO ILI KUHAKIKISHA WANANCHI WANASHEREKEA KWA AMANI NA UTULIVU TUMEIMARISHA DORIA ZA MIGUU, PIKIPIKI NA MAGARI KATIKA MAENEO YOTE MAJINI NA NCHI KAVU. AIDHA, NIMARUFUKU KUFANYA MIKESHA YA MAKONGAMANO NA MIKUTANO MAENEO YA WAZI, BADALA YAKE IFANYIKE KWENYE NYUMBA ZA IBADA AMBAPO MWISHO NI 00:30HRS USIKU NA HII NI KWA SABABU ZA KIUSALAMA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUTOSAHAU WAJIBU WAO NA KUWAACHA WATOTO KWENDA PEKEYAO KWENYE MAENEO YA MIKUSANYIKO KAMA; BARABARANI, SEHEMU ZA MICHEZO MFANO MAENEO YA BEACH/MIALO, DISKO TOTO NA KWENYE BEMBEA BILA UANGALIZI.
PIA NI MARUFUKU KWA MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO KUENDESHA WAKIWA WAMELEWA AU MWENDO KASI, ENDAPO IKIBAINIKA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO NA KWA WALE WENYE TABIA YA KUCHOMA MATAIRI BARABARANI WAACHE MARAMOJA KWANI NI KOSA KISHERIA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKIA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MWANZA NA WATANZANIA KWA UJUMLA SIKUKUU NJEMA YA MWAKA MPYA. LAKINI PIA KUSHEHEREKEA SIKUKUU HIYO KWA AMANI NA UTULIVU.