Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya kompyuta 50 zilizotolewa na Benki ya CRDB katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma.
Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Dkt. Benson Ndiege akitoa taarifa juu ya hafla ya makabidhiano ya kompyuta 50 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwenda kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa CRDB Prosper Nabaya akiongea kwa naiba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo mara baada ya kukabidhi kompyuta 50 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwenda kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika ,Collis Nyakunga akitoa neno la shukrani mara baada ya hafla ya kukabidhiwa kompyuta 50 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwenda kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja na Watumishi wa Benki ya CRDB wakifuatilia hafla ya kukabidhiwa kompyuta 50 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwenda kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB nchini Prosper Nambaya akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya kompyuta moja ikiwa ni sehemu ya kompyuta 50 zilizotolewa na Benki hiyo kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika Tanzania Dkt. Benson Ndiege kompyuta alipokea kutoka kwa Benki ya CRDB Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa makabidhiano ya kompyuta 50 zilizotolewa na Benki ya CRDB katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma
…………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya leo amekabidhi kompyuta 50 kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini(TCDC) zilizotolewa na Benki ya CRDB, huku akiagiza kuongezwa kasi ya kushughulikia maombi ya leseni ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo(Saccos).
Akikabidhi vifaa hivyo, Kusaya amesema matarajio ya serikali ni kuona kompyuta hizo zinaongeza kasi ya uwajibikaji kwa watumishi wa Tume hiyo ikiwamo kutoa leseni na utendaji kazi wao utapimwa kupitia vifaa hivyo.
Ameeleza kuwa kutolewa kwa kompyuta hizo kutasaidia ofisi kusimamia utoaji wa leseni ambazo zinaombwa na kutolewa kwa njia ya mtandao.
“Mnapaswa kuongeza ufanisi katika upatikanaji, utunzaji na utoaji wa taarifa na takwimu mbalimbali za vyama vya ushirika kama vile idadi ya vyama, wanachama, hisa, mtaji , ukaguzi, usajili, uwekezaji, masoko, madeni na migogoro,”amesema.
Ameitaka Tume hiyo kuhakikisha inatunza ipasavyo na kutumika vizuri ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Ameishukuru CRDB kwa vifaa hivyo huku akitoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kuiga mfano huo wa kutoa sehemu ya mapato yao kununua kompyuta hizo.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo na Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk.Benson Ndiege, amesema kukosekana kwa vitendea kazi ikiwamo kompyuta na vyombo vya usafiri kumesababisha vyama vya ushirika kutokaguliwa mara kwa mara.
Naye Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa CRDB Prosper Nabaya amesema kuwa Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika na kuongeza kuwa hadi sasa Benki hiyo imewakopesha Wakulima walio kwenye Vyama vya Ushirika zaidi ya bilioni 650.
“Katika mwaka wa fedha wa 2019/20 Benki ya CRDB imetoa jumla ya mikopo ya kilimo ya shilingi bilioni 650 sawa na asilimia 40% ya mikipo yote ya kilimo nchini Tanzania. Kati ya mikopo hiyo bilioni 495 imeelekezwa kwenye mazao makuu ya kimkakati hivyo kumsaidia zaidi ya AMCOS 472 kupata mikopo kwa ajili ya kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo (mikopo ya pembejeo, maghala, ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao, mikopo kwa ajili ya miradi ya ufugaji, uwekezaji kwenye misitu na mazao yake pia uwekezaji kwenye uvuvi.” ameeleza Nambaya.