Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya – Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ULRICH O. MATEI.
Mkaguzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Kanda ya Nyanda za Juu Kusini – GRACE KAPANDE.
*******************************************
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu 1. MWAPI ERASTO [36] Mkazi wa Iyela 2. DURGA RAJU [29] Mkazi wa Uhindini na 3. FREDY NGUVILLA [56] Mkazi wa Pambogo jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na boksi 541 za dawa binadamu aina mbalimbali zilizoisha muda wa matumizi.
Ni kwamba mnamo tarehe 30/12/2020 majira ya jioni, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipata taarifa toka kwa raia mwema na kufanya msako mkali huko maeneo ya Ilembo Jijini Mbeya na katika nyumba ya kulala wageni iitwayo “UWANJI GUEST HOUSE” iliyopo pambogo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu.
Katika upekuzi uliofanyika katika nyumba hizo tulifanikiwa kukamata maboksi 553 ya dawa za binadamu aina mbalimbali zilizoisha muda wake yenye thamani ya Tshs.171,137,200/=. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
Dawa hizo ni pamoja na:-
- BENZATHINE BENZYL PENCILLINE 2.4
- BENZATHINE DENCILLINE INJ-39 C1950
- AMPICILLINE INJ 758 VIALS
- TENOFOVIR / LAMIVUDINE
- SALBUTAMOL INHALOR
- MEBENDAZOLE TABS – 15 TINS OF 100 TABS
- ZIDOVUDINE / LAWIDINE / NEVIRAPINE TABS
- BETAMETHASONE EAR / EYE DROP
- BENZATHINE BENZYLPENCILLIN SODIUM INJ