Na Ahmed Mahmoud Simanjiro
Chama Cha wachimbaji wa Madini ya Tanzanite Mkoa wa Manyara MAREMA,tawi la Mererani, kimetoa tamko la kulaani taarifa inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii ikimhusisha waziri wa Madini Doto Biteko na mameneja wa migodi kupanga njama za kuhujumu Madini kinyume Cha Sheria.
Akiongea na vyombo vya habari Katibu wa MAREMA tawi la Mererani,Recho Joseph alidai kwamba taarifa hiyo ambayo inasambaa kwenye magroup mbalimbali yakiwemo ya ccm Ina lengo la kumchafua waziri ambaye amekuwa mstari wa mbele kudhibiti utoroshwaji wa Madini.
Alisema kripu hiyo inawataja mameneja wawili wa migodi ya Madini ya Tanzanite ambao ni Omari Mandal meneja wa Mgodi wa California na Joel Saitoti meneja wa Mgodi wa Gem and Rock Venture .
Wakidaiwa kukutana na waziri Biteko jijini Dodoma na kupanga njama za kuhujumu Madini yatakayopatikana wakati mameneja hao wakiwakagua wafanyakazi wao wanapokuwa wanatoka kwenye mgodi na Madini hayo yakipatikana atapatiwa waziri huyo kinyume na utaratibu .
“Hii Kripu inayosambaa inamtuhumu Saitoti na Omari kuwa walienda Mjini Dodoma na kukutana na waziri Biteko kwa lengo la kumshawishi aje kutoa tamko la kuwataka mameneja wa migodi kuanza kuwakagua wachimbaji pindi wanapotoka mgodini ili mawe yatakayopatikana yatoroshwe na kukabidhiwa waziri Biteko “Alisema Recho
Awali waziri Biteko ,Desemba 16 mwaka huu alitua Mjini Mererani na kufanikiwa kukutana na wamiliki wa migodi na wachimbaji na kutoa maelekezo kwamba mameneja wa migodi wahusike kuwakagua wachimbaji wao kabla hawajakaguliwa lango kuu na atakayekutwa na Madini mgodi mgodi wa mhusika .
Inadaiwa kauli hiyo ilizua taharuki kwa wachimbaji wakiwemo wachuuzi wa Madini (wanaapolo) na kuwatuhumu mameneja hao wa migodi kusuka mpango huo kwa waziri.
Kwa upande wake Omari Mandal alikanusha vikali kuhusika na mpango huo akidai unalenga kumchafua waziri kwani wao hawajawahi kukutana na waziri Biteko jijini Dodoma kwa ajili ya Mambo ya wachimbaji Mererani japo alikiri kwenda Dodoma kwenye masuala yake ya Kilimoa
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro,Awadhi Omari alisema kuwa group la ccm wazalendo ambalo Kripu hiyo ilitumwa huko ,chama Cha mapinduzi hakihusika ila watu wanataka kuchonganisha chama na serikali .
Alisema ccm itaendelea kufuatilia ili Kama itabainika kwamba waliohusika kusambaza ujumbe huo kupitia magroup ya ccm ni wanachama wa ccm,chama kitachukua hatua.