Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Wachezajia pamoja na Makocha wa zamani katika kikao alichokiongoza kuhusu maendelo ya michezo nchini. Kikao hicho kilifanyika Desemba 28, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na Wachezajia pamoja na Makocha wa zamani katika kikao alichokiongoza na Mhe. Waziri Bashungwa (hayupo pichani) kuhusu maendelo ya michezo nchini. Kikao hicho kilifanyika Desemba 28, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wakitoa maoni katika kikao cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa na Wachezaji pamoja na Makocha wa zamani kuhusu maendelo ya michezo nchini. Kikao hicho kilifanyika Desemba 28, 2020 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati), Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega wakiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji pamoja na Makocha wa zamani baada ya kikao kuhusu maendelo ya michezo nchini. Kikao hicho kilifanyika Desemba 28, 2020 Jijini Dar es Salaam.
*******************************************
Na Shamimu Nyaki –WHUSM,Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha heshima ya michezo hapa nchini inarejea.
Mhe. Bashungwa ameyasema hayo Desemba 28,2020 Jijini Dar es Salaam ambapo alifanya kikao na makocha pamoja na wanamichezo wa zamani na ameeleza kuwa Serikali imeanza kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Michezo.
“Lengo la kikao hiki ni kupokea mawazo kutoka kwenu namna bora ya kuendesha michezo ili tupate mafanikio kama ambayo tulipata hapo zamani wakati nyie mkilitumikia taifa letu katika soka” alisema, Mhe. Waziri Bashungwa.
Mhe. Bashungwa ameongeza kuwa marekebisho yaliyofanywa katika Sheria za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya mwaka 1967 kuhusu michezo ya ridhaa na kulipwa, Kwa hivi sasa inatambua michezo ya kulipwa ambapo kuna wachezaji zaidi ya 2000 wanaocheza michezo ya kulipwa ndani ya nchi na wanamichezo takriban 28 wanacheza michezo ya kulipwa nje ya nchi.
Aidha, Mhe. Waziri Bashungwa amewapongeza wachezaji wa zamani kwa jinsi walivyojituma kwa nidhamu na moyo wa kizalendo kuipigania nchi na kufanikiwa kufuzu katika mashindano ya AFCON mwaka 1979.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega ameiagiza Idara ya Michezo kusimamia maazimio yote ya kikao hicho kufanyiwa kazi na matokeo yaonekane.
“Nia yetu ni kuendeleza michezo, na hili tutalisimamia vyema hivyo tunaomba mawazo mazuri kutoka kwenu namna ya kuendeleza michezo” alisema Mhe.Ulega.
Mhe. Ulega ameongeza kuwa dhamira ya vikao na wadau wa michezo ni kutathmini michezo ilipotoka, ilipo na wapi ielekee kwa maslahi ya taifa.
Naye Mdau wa michezo michezo Bw. Ally Mayai Tembele ameishukuru Serikali kwa kuandaa vikao vya kukutana na wadau kupokea mawazo kuhusu maendeleo ya michezo nchini, huku akieleza kuwa michezo inahitaji nidhamu na kuwekeza kwa Watoto wa shule za msingi na sekondari, vifaa vya michezo na miundombinu bora ya michezo.