Moto umeunguza maduka zaidi ya 10 na kuteketeza baadhi ya vitu ni katika majengo yanayomilikiwa na familia ya Nekemia Kazimoto (Kazikomu) yaliyopo Mji wa kayanga mjini, Karagwe, Kagera mkabara na majengo ya city center na Magereza ya kayanga, moto umeibuka saa 5 na dakika 20 usiku katika moja ya duka la nguo na kusambaa katika maduka mengine ya bidhaa za vyakula, hoteli, stoo za vifaa vya ujenzi, salooni na maduka ya bidhaa mchanganyiko. moto umedumu zaidi masaa manne na chanzo cha moto hakijafahamika mpaka sasa. 26 Disemba 2020. Picha na Eliud Rwechungura