Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza amefariki dunia usiku huu wa leo Disemba 24, 2020.
Taarifa za awali zinaeleza amefariki akiwa jijini Dodoma, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi.
Tutaendelea kukupa taarifa zaidi kuhusu msiba huu