Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akiwa katika Studio za E FM Redio kwenye kipindi cha Uhundo leo Desemba 23, 2020 akizungumzia Maandalizi ya Tamasha la Serengeti Festival litakalofanyika tarehe 26,Desemba 2020, ambapo alieleza kuwa kwa wasanii watakaokosa nafasi katika tamasha hili kuwa wasijali watapewa nafasi katika tamasha lijalo mwakani
Msanii wa Bongo Fleva Faustine Mfinanga maarufu kama Nandy akieleza kuwa amajipanga kisawasawa na katika siku hiyo atazindua wimbo wake wa Singeli katika Tamasha la Serengeti Festival litakalofanyika tarehe 26,2020 hivyo mashabiki zake wajipange kupokea wimbo huo kupitia jukwaa hilo, leo Desemba 23,2020 katika Studio za EFM Redio kwenye kipindi cha Uhondo akiwa amembatana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi kuzungumzia maandalizi ya tamasha hilo.
Msanii wa Bongo Fleva Pamela Dafa maarufu kama Nandy akieleza kuwa amejipanga vizuri sana kutoa burudani ya kutosha kwa mashabiki zake katika Tamasha la Serengeti Festival litakalofanyika tarehe 26,2020 hivyo mashabiki zake, leo Desemba 23,2020 alipokuwa Studio za EFM Redio kwenye kipindi cha Uhondo akiwa amembatana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi kuzungumzia maandalizi ya tamasha hilo.
************************************
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
23/12/2020.
Tamasha la Serengeti Music Festival nila Kitaifa na kwa Wasanii watakao kosa nafasi katika tamasha hili la tarehe 26 Desemba, 2020 wasijali watapata nafasi mwakani katika tamasha lijalo.
Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 23, 2020 na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi katika Studio za E FM Redio katika kipindi cha Uhondo ambapo alifika kuelezea maandalizi ya tamasha hilo linalofanyika hivi karibuni pamoja na tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika tarehe 27,Dsemba 2020 baada ya tamasha hilo.
Akizungumza katika kipindi hicho alisema jina la Serengeti katika tamasha limekuja kwa lengo la kuileta karibu sekta ya Sanaa na Utalii pamoja kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii.
“Kutokana na ukubwa wa tamasha hili kwa mwakani tunaweza hata kulifanya ndani ya mbuga ya Serengeti kwa lengo tu la kutangaza utalii wa mbuga hii iliyojitwalia tuzo nyingi kimataifa na kuipa heshima nchini kwa kutangazwa kuwa ni moja ya kivutio ambacho kinaweza kutembelewa na watalii wengi,”alisema Dkt.Abbasi.
Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali aliongeza kuwa siku hiyo ya tamasha ni siku ya kusheherekea vipaji vya wasanii wa Tanzania kwani Sanaa nchini imekuwa kutoka kuonekana kama jambo la kihuni mpaka kuonekana kama biashara. Ambapo alieleza wasanii wengi Bongo Fleva na Hip Pop wa zamani watashiriki kutoa burudani kwa mashabiki zao.
Aidha, Katika mahojiano kuhusu hayo wasanii watatu ambao watashiriki tamasha hilo ambao ni Nandy, Lina na Pam D, .
Naye msanii wa Bongo Fleva Nandy alitoa msisitizo kwa wasanii wenzake kujipanga kweli kweli kutokana na tamasha hilo kuwa ni kubwa, huku akiwasihii watanzania wengi na kujitokeza katika tamasha hilo kwani hajawahi kutokea katika tamasha moja kuwa na wasanii zaidi ya 40 hivyo hiyo ni bahati kubwa.
“Nina nyimbo yangu ya Singeli nafikiri nitaizindua katika tamasha hili hivyo mashabiki zangu hii siyo ya kukosa,”alisema Nandy.
Halikadhalika nae msanii mwanadada Pam D alisisitiza kuwa amejipanga vizuri sana na mashabiki zake wajiandae kupata burudani ya hakika ya kufunga mwaka.
Sambamba na hayo Dkt.Abbasi alieleza kiingilio ni Tsh. Elfu tano na tiketi zinakatwa kupitia mfumo wa N-Card na kadi hizo zinapatikana maeneo mbalimbali ikiwemo Merere Sports Wear Kariakoo, Sunderland Sports Wear Kariakoo/ Nyamwezi,Maduka yote ya Vunja Bei, Shafii Dauda Tabata/ Sinza pamoja na Uwanja wa Uhuru mpaka kipindi cha Tamasha.