************************************
Klabu ya Yanga yaendeleza kutembeza kichapo katika ligi Kuu Vodacom Tanzania bara baada ya kuichapa Ihefu Fc mabao 3-0 na kuendelea kujikita kileleni.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke dakika 13, Yacouba 50 na Feisal dakika 60 na kumalizika kwa mchezo Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.