Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Watendaji wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (hawapo pichani) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi (hawapo pichani).Ziara hiyo imefanyika Desemba 23, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania Bi Doreen Sinare (aliyesimama) wakati viongozi hao walipoitembelea Taasisi hiyo Desemba 23, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na Watendaji wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (hawapo pichani) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo akiwa Waziri wake Mhe. Innocent Bashungwa pamoja Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi (hawapo pichani). Ziara hiyo imefanyika Desemba 23, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Watendaji wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (hawapo pichani) katika ziara ya Mhe Waziri Innocent Bashungwa na Naibu wake Mhe. Abdallah Ulega.Ziara hiyo imefanyika Desemba 23, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Taasisi hiyo wakati viongozi hao walipoitembelea Desemba 23, 2020 Jijini Dar es Salaam.
***********************************************
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameiagiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuongeza kasi katika kutekeleza usimamizi wa kazi za Sanaa.
Mhe. Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Desemba 23, 2020 Jijini Dar es Salaam alipotembelea Taasisi hiyo akiambatana na Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi.
Katika ziara hiyo Mhe. Bashungwa ametoa wiki moja kuanzia leo kwa Taasisi hiyo kuhakikisha wanakuwa na Mpango Mkakati wa namna ya kushughulika na waharamia wa kazi za Sanaa.
“Nawaagiza COSOTA kujitangaza kutumia vyombo vya habari na njia nyingine ikiwemo Mitandao ya kijamii ili mnayotekeleza wadau wenu wayajue” alisema, Waziri Bashungwa.
kwa upande wake Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega ameiagiza Taasisi hiyo kuongeza juhudi katika kukusanya mapato ya Serikali kupitia sekta ya Sanaa.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Hassan Abbasi ameeleza kuwa, tangu COSOTA ihamie Wizara ya hiyo mabadiliko mbalimbali yaliyohotajika kufanyika yametekelezwa, huku akiongeza kuwa lengo ni kuhakikisha Wadau wa Sanaa wananufaika na kazi zao.
Vile vile Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kuhuisha muundo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wasanii.