****************************************************
Leo 23/12/2020 kikao cha Kwanza cha baraza la Madiwani la Jiji la Dar es salaam kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Baraza la madiwani katika Jiji la Dar es Salaam.
Katika kikao hicho madiwani wote (WAJUMBE) wa Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. OMARY ABDALLAH MATULANGA walikula kiapo cha uaminifu na kiapo cha maaadili.
Mara Baada ya kiapo hicho Mstahiki Meya alianza Kwa kumshukuru Mungu kwa kuwapa uhai na kusimamia michakato yote mpaka kukamilika kwa wao kuapa,
pia ndg Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe Omary Matulanga amewapongeza watumishi wote wa Jiji wakiongozwa na mkurugenzi wa Jiji kwa kusimamia utendaji kipindi chote ambacho Baraza halikuwepo pamoja na kuahidi ushirikiano kwa kipindi chote cha uongozi wake.
Alisema ” Nitoe shukurani kwa watumishi wote wa Jiji wakiongozwa na mkurugenzi wa Jiji kwa kusimamia vema jiji letu na naahidi kwa niaba ya madiwani wote tutawapa ushirikiano wa kutosha kipindi chote cha uongozi wangu. “
Aidha Mhe Matulanga ametoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayo ongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya kimkakati katika Jiji la Dar es Salaam yenye lengo la kurahisisha maisha bora kwa kila mtanzania na kuahidi katika kipindi Chote cha uongozi wake kitakwenda sambamba na Kasi ya serikali hiyo katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Kipindi cha 2020-2025 katika Halmashauri ya jiji la Dar Es Salaam.