******************************************************
Mwandishi wetu,Babati
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amekabidhi baiskeli 31 kwa walemavu zenye thamani ya sh 21 milioni.
Baiskeli hizo zimetolewa na Taasisi ya uhifadhi ya chemchem ambayo imewekeza Utalii wa picha na hoteli Wilayani Babati.
Akizungumza leo Desemba 22wakati akikabidhi Baiskeli hizo, Mkirikiti alishukuru taasisi ya Chemchem kutoa Msaada huo na kutaka iendelee kusaidia jamii mkoa wa Manyara.
“Tunashukuru kwa Msaada huu lakini isiwe mwisho endeleeni kutoa kama mchango wenu kwa jamii na mimi leo ntatoa mchele kwaajili wa sikukuu kwa walemavu hawa pia fedha kidogo za kuwasaidia”Amesema
Mkurugenzi wa chemchem Nicolas Negri amesema Msaada huo ni sehemu ya baiskeli 242 ambazo wanakusudia kutoa kwa walemavu.
“Biashara yetu kubwa sisi ni Utalii hivyo kama tukiendekea kuhifadhi mazingira na kutunza wanyama tutaendelea kupata Watalii na kunufaika wote” amesema
Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara ina jumla ya walemavu 1811 wa aina mbalimbali ikiwepo walemavu wa viungo 249.