Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji TCRA Bw. John Daffa akizungumza katika mahafali ya 9 ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, yaliyofanyika leo Chuoni hapo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu VETA Bw.Mesai Msengi akizungumza katika mahafali ya 9 ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo VETA Kipawa Mhandisi Sospeter Mkasanga akizungumza katika Mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo leo Jijini Dar es Salaam.
Bw.Nelson Rutta akizungumza kwa niaba ya wazazi walioweza kufika katika mahafali ya 9 ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA,yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakiwa katika mahafali ya 9 ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji TCRA Bw. John Daffa akimtunuku cheti mhitimu wa Chuo VETA Kipawa katika mahafali ya 9 ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, yaliyofanyika leo Chuoni hapo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji TCRA Bw. John Daffa akipata picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wahitimu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA katika mahafali ya 9 ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA,
*****************************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, ina mpango wa kujenga kiwanda cha kutengeneza simu nchini ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa wahitimu kwa ngazi ya Ufundi stadi nchini.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa leseni na ufuatiliaji kutoka TCRA, Bw.John Daffa Wakati wa mahafali ya 9 ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam ambapo zaidi ya wanafunzi 200 wamehitimu kutoka kwenye Taaluma mbalimbali yenye mchepuo wa TEHAMA .
“Ujenzi wa kiwanda hicho unatazamiwa kuanza mwakani ikiwa lengo ni kusaidia kupunguza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi ambayo ajenda yake ikiwa ni ya viwanda huku wanufaika wakuu wakiwa ni wahitimu kutoka VETA”. Amesema Bw.Daffa.
Aidha amesema TCRA inampango wa kuondoa mafundi vishoka wa kutengeneza simu kwani wameshaanza kutoa leseni kwa wategenezaji wa simu nchini kwa ambao wamekidhi vigezo kutoka vyuo husika ambavyo ni VETA na Taasisi ya Teknolojia (DIT).
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Mhandisi Sospeter Mkasanga, amesema kuwa ujio wa kiwanda cha kutengeneza simu kwao utaongeza wigo mkubwa wa kutoa elimu huku akidai kuongeza idadi ya wanafunzi kwa mwaka ujao wa masomo katika Chuo hicho.
Aidha Mhandisi Mkasanga amesema Chuo hicho kilifanikiwa kudahili wanafunzi 125 katika mafunzo ya muda mrefu kwenye fani mbalimbali kama vile umeme, Tehama na Elektroniki wahitimu 121 (wanawake 27 na wanaume 94).
Pamoja na hayo ameiomba TCRA kuhamasisha makampuni ya simu kama vile Samsung,Nokia Tecno, Huawei kutumia chuo hicho kwa kupeleka vifaa vya simu, tehama na elektroniki kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambapo itakuwa ni msaada kwa mafundi na wanachuo kwa ujumla.
Hata hivyo katika changamoto amesema gharama kubwa ya upatikanaji wa vifaa vya kiteknolojia kunapunguza kasi ya chuo hicho kuweza kutoa mafunzo yanayohitajika kwenye soko kwa wakati husika.
“Hii inapelekea kuendelea kutumia vifaa na mashine zilizopitwa na wakati kufundishia na kuathiri ubora wa ujuzi anaoupata mwanafunzi ukilinganisha na mahitaji ya soko”. Amesema Mhandisi Mkasanga.
Awali wakisoma Risala wahitimu wa chuo hicho wamiomba TCRA kuwasidia kuwatatulia baadhi ya changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo mabadiliko ya mitaala kuendana na kasi ya sayansi na Teknolojia,Muendelezo wa kozi ndefu,Upungufu wa vitabu kwenye Library ya chuo,Ukosefu wa vimbweta na Kukosekana kwa maeneo ya kufanya vitendo.
Nae Bw.Nelson Rutter akiongea kwa niaba ya wazazi amewataka wahitimu kuwa na nidhamu kazini ama kwa wateja wao ili kuweza kuunda uwaminifu kwani b aadhi ya mafundi wamekuwa si waaminfu kwa wateja wao.
Chuo cha TEHAMA cha VETA –kipawa ni moja kati ya vyuo vilivyopo nchini vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ambacho ni chuo cha mfano kinachotoa mafunzo mbalimbali yenye mchepuo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).