Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote (Wapili kusho) akimsikiliza mtaalamu (hayupo pichani) aliyekuwa akielezea masuala mbalimbali kuhusu ujenzi wa mradi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere alipotembelea mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akifurahia jambo na wadau wengine walioenda kutembelea na kujifunza katika mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote kiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka sekta ya elimu walioenda kutembelea mradi huo.
Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeeleza jinsi inavyojivunia na mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere ambalo baada ya kukamilika kwake hapo Juni 2022 linatarajiwa kuzalisha Migawati 2115 za umeme.
Haya yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote alipotembelea mradi huo ambao kwa ndio mradi pekee mkubwa wa umeme kwa sasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ameongeza kuwa mradi huu sio tu ni muhimu kwa Tanzania bali utazinufaisha pia nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi zingine jirani. Mhandisi Mlote pia ameeleza kuridhishwa kwake na ushiriki wa Watanzania katika katika ujenzi wa mradi huo, ambapo kati ya Wafanyakazi zaidi ya 5000, asilimia 90 ni Watanzania.
Eng. Mlote ameonesha furaha yake baada ya kuelezwa kuwa mradi huo mkubwa Afrika Mashariki kwa sasa unafadhiliwa na Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimi 100, chini ya Uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli. Mhandisi Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo mradi wa kutunza mazingira ili kuufanya mradi huo kuendelea kuwa katika mazingira mazuri na salama wakati wote.
Awali ujumbe huo wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo na kueleza kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vilevile ametumia fursa hiyo kuwasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujuzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza miradi hata baada ya wataalmu kutoka makampuni yanayohusika na ujenzi kuondoka nchini.