***********************************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Yanga imeendelea kufanya vizuri kwenye ligi ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kufanikiwa kuichapa Dodoma Jiji mabao 3-1 katika dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Dodoma Jiji ilianza kutangulia kupata goli kupitia kwa Seif Karihe dakika ya 3 ya mchezo baada ya kutumia vizuri madhaifu ya kipa wa Yanga Metacha Mnata.
Magoli ya Yanga yaliwekwa kimyani na Lamine Moro dakika 27, Saidi Ntibazonkiza dakika 69 huku goli la tatu likifungwa na na Bakari Mwamnyeto dakika 75.
Kwa matokeo haya Yanga inaendelea kuongoza ligi ikifanikiwa kujinyakulia pointi 40 katika mechi 16.