Zanzibar 

Chama cha AAFP kimesema ili maridhiano yaliofikiwa Zanzibar  yalete manufaa kwa jamii vyama vingine vya siasa vishirikishwe kuondosha hofu ni makubaliano kati ya CCM na ACT  Wazalendo.
Pia kimedai ni busara nafasi kumi  za  uteuzi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa baraza la Mapinduzi  tano vikapewa vyama vilivyoshiriki Uchaguzi mkuu.
Hayo yameelezwa na Makamo Mwenyekiti  wa AAFP Omar Juma Said  aliyesema maridhiano hayo endapo yatabaki kwenye sura ya sass yanaweza kupoteza afya na kutoheshimika. 
Omar amesema maridhiano ni jambo jema katika jamii hivyo dhamana hiyo isiwe imebebwa aidha na wanasiasa au vyama viwili. 
Amesema kasoro  au dosari  zinazotokea zanzibar haziachi athari kwa vyama viwilo badala yake  yamapozuka majanga   huwaumiza wafuasi wa CCM ,ACT  wazalendo na wa  vyama vingine   
Amesema maridhiano yaliofikiwa zanzbar  hayapendezeshi. Kuonelana ni ya CCM na ACT Wazalendo na kuviweka kando vyama vingine .
Omar amesema CUF na CCM toka mwaka 1995  kimeshiriki katika muafaka lakini sasa hakishirikishwi jambo ambalo amesema si sahihi.
Amesema huo ni katika udhaifu unaonyesha kubibagua baadhu ya vyama vinavyodhaniwa  vidogo wakati hakuna chama kidogo mbele ya sheria.
Omar amesema oinapotumika jina maridhiano ya Zanzibar  wakati ni  ya vyama viwili kwa niaba ya Zanzibar na watu wake, ameziita  hizo ni rafu za kisiasa.
Aidha Makamo  Mwenyekiti  wa AAFP  amestushwa na matamshi ya makamo wankwanza wa Rais Maalim  Seif sharif Hamad aliyesisitiza dhamira ya Act wazalendo ya  kuendelea na mashitaka yale icc haijafutika.
Amesema Ikiwa   kweli vyama hivyo vimefikia maridhoano ya dhati na kweli kuendeleza mashitaka hukobicc ni jambo linalozidisha hofu.