**************************************
19/12/2020 GEITA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi limeendelea kupata mafanikio makubwa ikiwemo kudhibiti vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha za moto huku akitaja mafanikio hayo yametokana na jitihada na weledi wa askari wa Jeshi hilo pamoja na ushirikiano kutoka kwa wananchi.
IGP Sirro amesema hayo leo Mkoani Geita wakati alipofanya ziara ya ukaguzi ambapo amekutana na makamanda wa mikoa mitatu ya Geita, Kagera na Kigoma na kufanya tathimini ya mafanikio yaliyotokana na juhudi za kudhibiti matukio ya uhalifu.
Aidha, IGP Sirro pia amekutana na askariu wa kikosi maalium cha kuzuia uhalifu ambapo askari hao walimuonyesha Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi silaha kadhaa za moto walizozikamata ikiwemo bunduki zilizotengenezwa kienyeji na kutumika kwenye matukio ya uhalifu