Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu sekta ya kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) uliopo Mji wa Serikali, Mtumba Disemba 18, 2020.
Mtaalam wa Rasiliamali Watu kutoka “Tanroads Engineering Consulting Unit (TECU) akieleza jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) uliopo Mji wa Serikali, Mtumba Disemba 18, 2020.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deo Ndejembi akieleza jambo wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato (kulia) wakati wa kikao hicho kilichowakutanisha kujadili kuhusu sekta ya kazi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng’i Issa akieleza jambo kuhusu suala la ushirikishwaji wa watanzania katika miradi ya serikali/ uwekezaji (Local Content) wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya Wajumbe wa kikao hicho wakisikiliza kwa makini maelezo ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) walipokutana kujadili sekta ya kazi nchini.
Kamishna wa Kazi, Brig. Gen. Francis Mbindi akifafanua kuhusu ushughulikiaji wa Vibali vya Kazi nchini wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) uliopo Mji wa Serikali, Mtumba Disemba 18, 2020. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Kazi, Bi. Lilian Francis.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato akieleza jambo wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu masuala ya kazi katika sekta ya nishati.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)