Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Suleiman Jafo, akionesha furaha wakati akikagua Stendi Kuu ya Mabasi ya Misuna ya Mkoa wa Singida jana. Kutoka kulia ni Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Singida, Bayona Lambati, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Mulagiri na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi.
Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Singida, Bayona Lambati, akitoa maelezo kwa Waziri Jafo wakati akikagua Stendi Kuu ya Mabasi ya Misuna.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Jafo wakati akikagua Stendi Kuu ya Mabasi ya Misuna.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Suleiman Jafo, akizungumza na Wananchi wakati akikagua Stendi Ndogo ya Majengo.
Muonekano wa Stendi Kuu ya Misuna.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Suleiman Jafo, akizungumza na waandishi wa habari wakati akikagua Stendi Kuu ya Mabasi ya Misuna ya Mkoa wa Singida. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi.
Wakala wa Mabasi katika stendi ya Misuna, Ibrahim Abdul akitoa pongezi kwa Serikali kwa kujenga stendi hiyo ambapo pia alimuomba Waziri Jafo kuzifanyia marekebisho barabara za pembezoni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Suleiman Jafo, akizungumza na wananchi wakati akikagua Stendi Kuu ya Mabasi ya Misuna ya Mkoa wa Singida. Kushoto ni Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Singida, Boniface William.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Suleiman Jafo, akizungumza na wananchi wakati akikagua Stendi ya Misuna..
|
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, akimuelekeza jambo Waziri Jafo. |
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Jonathan Semiti, akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Suleiman Jafo, baada ya kukagua Stendi Kuu ya Mabasi ya Misuna.
Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Singida, Boniface William (kulia) wakizungumza jambo na Afisa wa Takukuru Wilaya ya Singida, Samsoni Julius baada ya Waziri Jafo kukagua Stendi ya Misuna. Katikati ni Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Singida, Bayona Lambati.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Suleiman Jafo ameupongeza Mkoa wa Singida kwa kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo iliyopo Manispaa ya Singida.
Alisema kipindi cha miaka mitano Serikali ilitoa Sh. Bilioni 24 mkoani hapa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Stendi Kuu ya Misuna, Stendi ndogo ya Majengo, ujenzi wa barabara za kiwango cha lami ndani ya Manispaa hiyo, taa za barabarani na ujenzi wa majengo katika stendi hizo.
Jafo alitoa pongezi hizo mkoani hapa jana wakati akipokea taarifa katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi hiyo.
“Ninawapongeza viongozi wote wa Mkoa wa Singida kwa kusimamia na kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa hongereni sana.” alisema Jafo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Lyapambile alisema ujenzi wa miradi hiyo yote uligharimu Sh. Bilioni 24 kati ya fedha hizo Sh. Bilioni 2.7 zilitumika kujenga stendi kuu ya Misuna na miundombinu yake yote.
Wakati huo huo Jafo alimpongeza Rais John Magufuli kwa kasi yake kubwa ya maendeleo yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya uongozi wake ambapo amejenga Hospitali 99, Vituo vya Afya 487 na Zahanati 1198 na kuweka kumbukumbu ya kihistoria hapa nchini.
Aidha Jafo alisema Serikali katika kipindi hicho cha miaka mitano imeweza kujenga stendi za mabasi katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Iringa, Rukwa, Katavi, Simiyu, Tanga na Singida.
Wakati huo huo Jafo amewataka viongozi na wananchi kuilinda miradi hiyo ambayo Serikali imetumia fedha nyingi kuijenga na kuwa mtu yeyote atakaye bainika kuihujumu atachukuliwa hatua kali za kisheria.