Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya
Mkoa huo (RCC), akiongoza kikao cha
kamati hiyo cha kujadili mambo
mbalimbali ya maendeleo mkoani humo, Desemba 17, 2020. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), wakiwa katika kikao hicho muhimu amacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Mafuru akielezea jinsi jiji liliyyojipanga |
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya
Mkoa huo (RCC), ameongoza kikao cha
kamati hiyo ambacho kimejadili mambo
mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Kamati hiyo ya ushauri inashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo
baadhi ya wakuu wa idara wa ofisi ya mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi
watendaji wa halmashauri, wabunge, wenyeviti wa
halmashauri na baadhi ya viongozi wa taasisi.
Awali wajumbe walithibitisha
muhtasari wa mambo yote yaliyopitishwa katika kikao kilichofanyika mwaka
jana Desemba 19, 2019
Katika kikao hicho wajumbe walijadili mada mbalimbali zilizowasilishwa za jinsi ya
kuboresha sekta ya elimu, sekta ya afya, tathmini ya hali ya chakula na maandalizi
ya kilimo msimu wa . 2020/21.
Pia, wajumbe walipitia
Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/20
na 2020/21 kufikia Noemba 2020, Mpango wa
Bajeti wa mwaka 2019/20 kufikia Novemba 2020 na mwelekeo kwa
mwaka 2021/22, mapato ya ndani ya Halmashauri na matumizi kufikia Novemba 2020.
Aidha,wajumbe walipatiwa taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge
na Madiwani Oktoba 2020, Taarifa ya
utekelezaji wa maazimio ya Kamati hiyo
ya Wakala kwa Huduma ya Misitu (TFS).
Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mahenge ameagiza TFS kuweka utaratibu wa kukagua mara kwa mara mwenendo
wa upandaji miti katika halamashauri zote ii kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Mkakati huo uhusishe viongozi wa ngazi zote, wakiwemo wakuu wa wilaya,
wakurugenzi wa halmashauri na viongozi wa mkoa.
Baadhi ya maagizo yaliyotolewa kwenye kikao ni; kuunda
Kamati ya Mkoa ya kufuatilia uboreshaji wa
elimu ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa Mkoa huo ambao kwa hivi sasa
unashika nafasi ya 22 kitaifa.
Dkt. Mahenge amewataka viongozi wote
wajenge umoja na ushirikiano kwa kuweka misingi imara ya kudumu ya kuinua kiwango cha elimu ambayo ni
ufundishaji bora, usimamizi, ufuatliaji na utawala.
Halmashauri zimetakiwa kuandaa vivutio vya uwekezaji,
kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji na
kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya ardhi kwa wawekezaji na hata
ikiwezekana kuingia ubia nao.