Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandishi Antony Sanga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov wakikata utepe kuashiria uzinduzi ramsi wa mradi wa maji wa Msamalo wilayani Chamwino-Dodoma.Mradi huo utatoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi zaidi 4,000 pamoja na taasisi za kijamii.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandishi Antony Sanga akimtwika ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Msamalo Wilayani. Chamwino mkoani Dodoma baada ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Msamalo ambao utahudumia kaya zaidi ya 730 pamoja na taasisi za kijamii zikiwamo shule, kliniki pamoja na taasisi za dini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Antony Sanga pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov wakinywa maji safi na salama kutoka kwenye mradi wa maji wa Msamalo uliozinduliwa jana.Mradi huo utasaidia kutoa mani safi na salama kwa wanakijiji zaidi ya 4,000 waishio kwenye eneo hilo.
**********************************
Dodoma.Desemba 16,2020. Shida ya maji kwa Wakazi wa Kata ya Msamalo,Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kwa sasa itabaki kuwa historia baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa maji utakaowanufaisha wakazi zaidi ya 4,000 pamoja na taasisi za kijamii kwenye eneo hilo.
Katika kuhakikisha idadi kubwa ya watu inafikiwa na huduma ya maji safi na salama, Shirika la Water Mission Tanzania kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) limezindua mradi huo ambao utapunguza adha ya kufuata maji umbali mrefu kwa wakazi 4,085 wa eneo hilo.
Pia, mradi huo utazinufaisha zaidi ya kaya 730 pamoja na taasisi mbalimbali za kijamii ikiwamo kliniki, masoko pamoja na taasisi za kidini jambo ambalo linaashiria ustawi wa watu pamoja na shughuli za kijamii na kiuchumi.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov alisema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata maji safi na salama karibu na makazi yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov alieleza kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na mfumo thabiti wa kupata maji safi na salama karibu na makazi yao.
“Tunatambua uwepo wa mahitaji makubwa ya maji kwenye eneo hili na leo hii tunayo furaha kuzindua mradi huu ambao utasaidia kupunguza adha ya maji kwa wakazi wa eneo hili.Mafanikio hay ani ishara ya ushirikiano wet una Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na Wizara ya Maji katika kusaidia jitihada za Serikali kufikisha huduma za maji kwa watu wote,” alisema.
Akizindua mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandishi Antony Sanga alisema kukamilika kwa mradi huo ni utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kupunguza kero ya maji kwa wananchi na kwamba utasaidia kuboresha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
“Tunamshukuru sana Rais wetu, wakati wa kampeni aliahidi kwamba tutawapelekea wananchi wetu huduma ya maji hivyo huu ni upendo wake kwenu wana Msamalo,” alisema.
Aliwataka wakazi wa Msamalo kushirikiana ili kuendeleza mradi huo ili uwe endelevu kwa manufaa kwa vizazi vijavyo.
Mradi huo unatumia nishati ya jua ‘Solar’ ambapo maji yanavutwa kutoka kwenye kisima na kwenda kwenye kituo cha kusafisha na kutibu maji na baadaye yanapelekwa kwenye vituo 18 vilivyopo karibu na makazi ya watu.