MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani kushoto akishauriana jambo na waratibu wa miundombinu ya mafunzo hayo |
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika Agri Thamani kushoto akiwa na Mratibu wa Agri Thamani Kagera |
Viongozi wa Serikali za mitaa wakifuatilia mafunzo hayo
Viongozi wa Serikali za mitaa wakifuatilia mafunzo hayo
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Shirika la Agri Thamani wametoa mafunzo ya lishe bora kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa
na Wajumbe wake kutoka Mitaa yote 66 ya Bukoba Manispaa mkoani Kagera.
Mafunzo haya yameandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya
Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba yakiwa na lengo kuhimiza suala la lishe bora kwenye
maeneo yao.
Shirika la Agri Thamani limeamua
kutoa mafunzo haya ikiwa ni jitihada ya kuhakikisha kuwa Viongozi hawa
wanachangia ipasavyo katika Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 ya
Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mhe Neema Lugangira
amesema kwamba kwa awamu ya kwanza Mafunzo hata yatatolewa kwenye Serikali za
Mitaa za Wilaya zitakazochaguliwa kutoka Mikoa mbalimbali nchini.
Mafunzo hayo yamewanufaisha viongozi 312 na kupitia Ushiriki
wao kama Viongozi kuanzia Ngazi ya Jamii huku akieleza Agri Thamani ina amini kama Taifa tutaweza
kufikia lengo la kuimarisha lishe bora nchini kama ilivyoainishwa kwenye Ilani
ya Uchaguzi ya CCM.