Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geofrey Mwambe (katikati) akisisitiza kusimamia azma ya serikali awamu ya tano ya kukuza uchumi wa viwanda kwa kuzingatia kuwa taifa limeingia uchumi wa kati,alipokuwa akizungumza na viongozi wa Menejimenti ya wizara hiyo (hawapo pichani) , leo Desemba, 17, 2020, katika kikao cha makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Innocent Bashungwa (wa kwanza kushoto) kilichofanyika leo Jijini Dodoma, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akiwasisitiza Viongozi wa Menejimenti wa wizara hiyo (hawapo pichani), kumpa ushirikiano waziri huyo mpya Mhe. Geofrey Mwambe (wa pili kulia) katika kikao cha makabidhiano ya ofisi kilichofanyika leo Desemba 17, 2020 Jijini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Ludovick Nduhiye.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Geofrey Mwambe kuzungumza na viongozi wa Menejimenti katika kikao cha makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Innocent Bashungwa, kilichofanyika leo Desemba 17, 2020, katika ofisi za Wizara hiyo, zilizopo Mji wa Serikali, Jijini Dodoma.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (wa kwanza kushoto) akikabidhi nyaraka za wizara hiyo kwa waziri wa mpya Mhe. Geofrey Mwambe (katikati) mbele ya viongozi wa menejimenti wa wizara hiyo (hawapo pichani) katika kikao cha makabidhiano ya ofisi kilichofanyika leo Desemba 17, 2020, katika ofisi za wizara hiyo zilizopo katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geofrey Mwambe (aliyesimama) akisisitiza kusimamia azma ya serikali awamu ya tano ya kukuza uchumi wa viwanda kwa kuzingatia kuwa taifa limeingia uchumi wa kati kwa viongozi wa Menejimenti ya Wizara hiyo, leo Desemba, 17, 2020, katika kikao cha makabidhiano ya ofisi kati yake na Waziri aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Innocent Bashungwa (wa kwanza kushoto) kilichofanyika leo Jijini Dodoma, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe.