*******************************
Mwili wa mfanyabiashara maarufu Mwenyekiti Mtendaji wa Motisun Group Subash Patel ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Subash Patel umezikwa leo katika makaburi ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akitoa ratiba ya shughuli nzima ya kuaga pamoja na mazishi Msemaji wa Makampuni ya Motisun Group, Bw. Aboubakari Mlawa alisema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na ameacha mke mmoja pamoja na Watoto wawili.
Bw. Patel alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi akiwa nyumbani kwake, Kisutu Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiendelea na matibabu.
Mfanyabiashara huyo maarufu nchini alikuwa akimiliki kampuni zinazotengeneza bidhaa za plastiki, saruji, mabati, nondo, nyaya za umeme, vinywaji, rangi na pia alimiliki hoteli za White Sands na Sea Cliff, Pearlsun Hotel & Resorts.
Via EATV