Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Mradi Ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma, Martin Pallangyo (kulia) kufanya kazi usiku na mchana ili jengo hilo linaloendelea kujengwa liweze kukamilika kwa wakati. Jengo hilo lenye ghorofa nane lilitakiwa kukamilika Mwezi huu Disemba, 2020 lakini mpaka sasa limefikia asilimia 41. Wapili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati) akimsikiliza Mkandarasi wa Mradi Ujenzi wa ofisi za Makao Makuu Uhamiaji jijini Dodoma, Martin Pallangyo alipokuwa anatoa maelezo ya mradi huo, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi huo, leo. Simbachawene hajaridhishwa na ujenzi wa jengo hilo, hivyo amemtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kulikamilisha jengo hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati) akiangalia paa la ghorofa ya tatu ya jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji linaloendelea kujengwa jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo, leo. Amemtaka Mkandarasi wa Meadi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kulikamilisha jengo hilo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Mradi Ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma, Martin Pallangyo (kushoto) kufanya kazi usiku na mchana ili jengo hilo linaloendelea kujengwa liweze kukamilika kwa wakati. Jengo hilo lenye ghorofa nane lilitakiwa kukamilika Mwezi huu Disemba, 2020 lakini mpaka sasa limefikia asilimia 41. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.